Issa Michuzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Muhidin Issa Michuzi ni mwandishi wa habari wa Tanzania anayejulikana kupitia blogu yake iitwayo Michuzi blog. [1]

Maisha yake na kazi[hariri | hariri chanzo]

Michuzi tangu zamani alikuwa akipendelea kazi ya upigaji picha. Mnamo mwaka 1980 alijiunga na vipindi vya jioni katika taasisi iitwayo Dar es Salaam. Moja kati ya picha alizowahi kupiga ilichaguliwa kwa ajili ya kurasa ya mwanzo wa gazeti la Daily News linalomilikiwa na serikali ya Tanzania.

Baada ya hapo aliajiriwa kwa mkataba wa muda mfupi kama ripota kwa muda wa miaka mitatu kabla ya kuajiriwa kwa mkataba wa muda mrefu Januari mwaka 1990.[2]

Mwaka 1992 alijiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari cha Ujerumani mjini Berlin Kwa masomo ya juu ya uandishi wa habari.Baadae alijiunga na chuo cha uandishi wa habari (present-day School of Journalism and Mass Communication) kilichopo University of Dar es Salaam na kumalza mwaka 1996.

Kazi yake ya uandishi[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Septemba 2005, Michuzi aliungana na Jakaya Kikwete ambaye kwa wakati huo alikuwa Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania aliyekuwa akihudhuria Mkutano wa Mchakato katika Utandawazi na Demokrasia mjini Helsinki nchini Finland. Huko likutana na Ndesanjo macha aliemsaidia kuandaa blogi yake.Blogi yake ya kwanza ailitengenezwa tarehe 8 seotemba mwaka 2005. [3] .Madhumuni yake yalikua kuwataarifu Watanzania kuhusu habari zinazohusu nchi yao kwa kupitia blogu za picha.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Michuzi ana kaka wawili, Ahmaad na Othman amabo pia wanashughulika na kazi zao na uandishi Tanzania.Kwa pamoja wametengeneza blogi iitwayo michuzi media Group (MMG).

Ni mpenzi wa muziki wa Tanzania bongo flava ni shabiki wa timu ya Liverpool F.C..

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.voaswahili.com/a/2955423.html iliangaliwa 21 Disemba 2019
  2. EXCLUSIVE INTERVIEW WITH TANZANIA'S MOST POPULAR BLOGGER ISSA MICHUZI! (May 2011). Iliwekwa mnamo 13 May 2013.
  3. Michuzi and Ndesanjo. Michuzi Blog (8 September 2005). Iliwekwa mnamo 13 May 2013.
Inkwell icon - Noun Project 2512.svg Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Issa Michuzi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.