Nenda kwa yaliyomo

Isaac Lenaola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Isaac Lenaola (alizaliwa Samburu, mnamo 21 Desemba 1967[1]) ni wakili na jaji wa Kenya, ambaye amewahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Kenya, tangu tarehe 28 Oktoba 2016.[2]

Historia na Elimu

[hariri | hariri chanzo]

Alianza masomo yake katika Shule ya Mtakatifu Mary huko Maralal, mnamo 1973. Aliendelea na masomo yake katika "Shule ya Msingi ya Maralal D.E.B." na "Shule ya Msingi Baragoi" ambapo alifanya mitihani yake ya Kumaliza Shule ya Msingi. Kuanzia 1981, alisoma katika Shule ya Upili ya Alliance kwa masomo yake ya kidato cha nne na kidato cha sita, akihitimu mnamo 1986, katika darasa lake, alipata alama bora zaidi katika elimu ya kidato cha sita nchini Kenya.

Mnamo 1987, Isaac Lenaola alijiunga katika Chuo Kikuu cha Nairobi, ambapo alisomea sheria, akihitimu na Shahada ya Sheria, mnamo 1990. Kisha akasoma katika Shule ya Sheria ya Kenya, ambapo alipata Mpango wa Mafunzo ya Mawakili.

Mwaka 1991 alijiunga katika Baraza la uanasheria nchini Kenya.

  1. KenyanLife (2016). "Biography of Isaac Lenaola, Justice of the Supreme Court of Kenya". Nairobi: Kenyanlife.com (KenyanLife). Iliwekwa mnamo 22 Agosti 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. PSCU (28 Oktoba 2016). "Judges Philomena Mwilu and Isaac Lenaola sworn in". Daily Nation. Nairobi. Iliwekwa mnamo 22 Septemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Isaac Lenaola kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.