Nenda kwa yaliyomo

Iodini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Iodini (Iodium)
Jina la Elementi Iodini (Iodium)
Alama I
Namba atomia 53
Mfululizo safu Halojeni
Uzani atomia 126.904
Valensi 2, 8, 18, 18, 7
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 386.85 K (113.7 °C)
Kiwango cha kuchemka 457.4 K (184.3 °C)
Asilimia za ganda la dunia 6 · 106  %
Hali maada mango

Iodini (kut. Kigiriki "Iodes" (ιώο-ειδης) "rangi ya dhambarau" kutokana na mvuke) ni elementi yenye namba atomia 53 katika mfumo radidia maana yake kiini atomia chake kina protoni 53. Uzani atomia ni 126.904 na alama yake ni I. Ni elementi ya nne katika safu ya halojeni.

Katika hali sanifu ni mango ya fuwele yenye rangi nyeusi-kijivu. Huanza kuvukamanga kuwa gesi kwa halijoto ya chumbani tayari. Kupata iodini kiowevu inawezekana kwa kuikanza haraka hadi kufikia kiwango cha kuyeyuka cha 113.7 °C.

Upatikanaji

[hariri | hariri chanzo]

Iodini yapatikana kwa wingi katika maji ya bahari pia katika madini mbalimbali.

Iodini na tezi ya shingo

[hariri | hariri chanzo]

Mwili wa kibinadamu huhitaji iodini; kwa kawaida viwwango vya kutosha hupatikana katika chakula cha kawaida. Isipokuwa katika maeneo kadhaa hasa mlimani uhaba wa iodini asilia husababisha magonjwa kama tezi ya shingo.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Matumizi yake ni katika madawa (hasa antiseptika), viungo vya chakula, rangi na kemia za kusafisha picha.

Iodini katika maji ni dawa antiseptika inayozuia maambukizo wa vidonda.

Uhaba wa iodini na matatizo yake

[hariri | hariri chanzo]

Watu wanahitaji kiasi kidogo cha iodini kwa miili yao na kwa kawaida wanakipata kupitia chakula au maji. Lakini katika maeneo pasipo na iodini katika mazingira asilia watu wanaona uhaba wa iodini unaosababisha maradhi kadhaa; matezi ya shingoni ni dalili la uhaba huu. Watoto wanaozaliwa na wakina mama wenye uhaba wa iodini hutokea mara nyingi kama vibete (watu wafupi). Pia akili za watoto wa wakinamama hao inaweza kupungukiwa. Mtoto aliyeathiriwa na uhaba huu haufikii kiwango cha akili kama watoto wengine.

Kwa sababu hii serikali katika nchi mblimbali zimeweka sheria za kutia kidogo sana iodini kwenye chumvi inayouzwa madukani.

Kwa upande mwingine iodini ni pia sumu kama kiwango chake kinazidi mahitaji ya mwali ambayo ni mikrogramu 100-200 tu kwa siku (mikrogramu ni sehemu ya milioni ya gramu).