Ilalambogo
Ilalambogo ni kijiji kilichopo kata ya Lubili, Wilaya ya Misungwi katika Mkoa wa Mwanza, Tanzania. Kimepakana na wilaya ya Nyang'hwale upande wa magharibi na kijiji cha Mabale upande wa kaskazini, kusini mwa kijiji hiki kimepakana na Mahando na mto Bukunga.
Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 5,691 waishio humo.[1] Msimbo wa posta ni 33508.
Ilalambogo imezungukwa na mlima Ilalambogo, mkondo wa Ziwa Viktoria pamoja na mto Bukunga unaotiririsha maji kutoka sehemu mbalimbali kwenda ziwani. Samaki aina mbalimbali wanapatikana katika mkondo wa ziwa Viktoria kama vile sato, kambale, gogogo na dagaa.
Ilalambogo kuna kivuko cha maboti madogo ya kwenda kijiji cha Kijinga wilaya ya Ng'wang'hale, mkoa wa Geita katika saa kumi na mbili.
Jamii ya watu wanaoishi ndani ya kijiji hicho ni Wasukuma ambao asilimia 90 ni wakulima na wafugaji. Wakazi wake ni wakulima wa mazao ya chakula na biashara, mazao ya chakula ni pamoja na mahindi, mtama, uwele, viazi vitamu, mpunga, maharagwe na mihogo. Mazao ya biashara ni pamoja na dengu, pamba, choroko na miwa kwa uchache.
Katika kijiji cha Ilalambogo kuna shule za msingi mbili ambazo ni Mwakitilyo na Ng'wang'handa.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ilalambogo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |