Nenda kwa yaliyomo

Ibrahim Hamad

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ibrahim Abdallah Hamad (maarufu kwa jina la Ibrahim Bacca,[1]; alizaliwa 12 Novemba 1997) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutokea nchini Tanzania anayecheza nafasi ya mlinzi wa kati kwenye klabu ya Young Africans S.C.. Anazichezea pia timu za taifa za Zanzibar na Tanzania.

Hamad alianza kucheza soka la kulipwa mwaka 2017 katika klabu ya Jang'ombe Boys F.C. inayoshiriki Ligi kuu ya Zanzibar. Alihamia Malindi S.C. mwaka 2019 na kucheza misimu miwili. Mwaka 2021, alihamia KMKM F.C. ambako alishinda taji la Ligi Kuu ya Zanzibar msimu wa 2021–22. Mnamo 14 Januari 2022 alihamia klabu ya Young Africans inayoshiriki NBC Premier League ambapo alishinda mataji ya ligi mara mbili mfululizo, Taji moja la Mashindano ya FA na Taji moja la Ngao ya Hisani.[2][3] Mnamo Novemba 2023 aliongeza mkataba wake mpaka mwaka 2027, baada ya kiwango cha hali ya juu alichokionyesha dhidi ya Al Ahly kwenye Mashindano ya Klabu bingwa Afrika, siku maalumu ilitengwa kwa ajili ya kumuenzi na kupewa jina la "Bacca Day".[4]

Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Hamad alitajwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar kwenye mashindano ya CECAFA mwaka 2017, ambapo timu yake ilimaliza nafasi ya pili.[5]

Mnamo tarehe 24 Machi 2023, alitajwa kwa mara ya kwanza kwenye kisosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania kenye mchezo dhidi ya Uganda katika mashindano ya kufuzu fainali za AFCON za mwaka 2023 ambapo walishinda goli 1 – 0.[6] Alikua katika kikosi cha mwisho kilichoiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya AFCON yam waka 2023.[7]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Hamad ni Muislamu mcha Mungu. Rafiki yake wa karibu alifariki katika ajali ya MV Spice Islander I mwaka 2011. Akiwa kijana, Hamad alifanya kazi ya kumenya viazi ili kuwathibitishia wazazi wake kwamba anaweza kufanya kazi. Alishawahi kuwa kwenye kikosi cha kuzuia magendo cha Zanzibar.[1]

KMKM
Young Africans
  1. 1.0 1.1 Olipa Assa (19 Mei 2023). "Bacca sio uaskari tu hadi chips kauza" [Bacca is not just a car for chips]. Mwananchi.co.tz. Ibrahim Abdallah Hamad 'Bacca' (24){{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "YANGA SC YASAJILI BEKI MAHIRI MZANZIBARI" [YANGA SC SIGNS UP A SMART DEFENDER FROM ZANZIBAR]. binzubeiry.co.tz.
  3. "Hawa hapa mastaa waliorejesha mataji Yanga" [Here are the stars who brought back Yanga titles]. Mwanaspoti.co.tz. 4 Februari 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "IBRAHIM BACCA AJITIA KITANZI JANGWANI HADI 2027" [IBRAHIM BACCA HAS A NOISE IN THE DESERT UNTIL 2027]. binzubeiry.co.tz.
  5. "Zanzibar's Football Heroes Win Hearts Despite Loss to Kenya in CECAFA Cup". 19 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Strack-Zimmermann, Benjamin. "Uganda vs. Tanzania". national-football-teams.com.
  7. "Maskauti wamganda Bacca, simu zinaita!" [The scouts have frozen Bacca, the phones are ringing!]. Mwanaspoti.co.tz. 25 Januari 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ibrahim Hamad kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.