Ngao ya Jamii
Ngao ya Jamii ni mashindano unaoashiria ufunguzi wa msimu mpya wa michezo yanayofanyika mara moja kwa mwaka unazozikutanisha mshindi wa msimu wa nyuma wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mshindi wa Kombe la FA Tanzania. Ikiwa mshindi wa Ligi kuu ndiye mshindi wa Kombe la FA, mpinzani atakuwa aliyeshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi. Mashindano hayo yanatambulika rasmi na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF).[1][2][3][4]
Mabadiliko ya Mfumo
[hariri | hariri chanzo]Kuanzia msimu wa 2022/23, TFF ilitangaza mabadiliko kwenye mfumo wa mchezo wa ngao ya Jamii. TFF ilbadilisha kanuni ya (19:1) kuhusu mchezo wa Ngao ya jamii ambapo kwa sasa kutakuwa na shindano la Ngao ya Jamii na sio mchezo mmoja[5]. Mfumo huu mpya unamaanisha kutakua na michezo ya nusu fainali na fainali. Michezo ya Nusu fainali ingezikutanisha Mshindi wa Ligi dhidi ya aliyeshika nafasi ya tatu kwenye msimamo, na Aliyeshika nafasi ya pili dhidi ya aliyeshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi. Timu za Young Africans, Simba, Azam na Singida big Starts ndizo zilizokua za kwanza kushiriki kwenye mfumo huu mpya, na Simba ndio timu ya kwanza kushinda taji la Ngao ya Jamii kwa kutumia mfumo huu.[6][7]
Washindi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Mshindi | Matokeo | Mshindani | Tanbihi. |
---|---|---|---|---|
2001 | Young African | 2–1 | Simba | |
2002 | Simba | 4–1 | Young African | |
2003 | Simba | 1–0 | Mtibwa Sugar | |
2004 | Haikuchezwa | |||
2005 | Simba | 2–0 | Young African | |
2006 | Haikuchezwa | |||
2007 | ||||
2008 | ||||
2009 | Mtibwa Sugar | 1–0 | Young African | |
2010 | Young African | 0–0
[3–1 pen] |
Simba | |
2011 | Simba | 0–0 | Young African | |
2012 | Simba | 3–2 | Azam | |
2013 | Young African | 1–0 | Azam | |
2014 | Young African | 3–0 | Azam | |
2015 | Young African | 0–0
[8–7 pen] |
Azam | |
2016 | Azam | 2–2
[4–1 pen] |
Young African | |
2017 | Simba | 0–0
[5–4 pen] |
Young African | |
2018 | Simba | 2–1 | Mtibwa Sugar | |
2019 | Simba | 4–2 | Azam | |
2020 | Simba | 2–0 | Namungo | [8] |
2021 | Young African | 1–0 | Simba | |
2022 | Young Africans | 2–1 | Simba | |
2023 | Simba | 0–0
[3–1 pen] |
Young Africans | |
2024 | Young Africans | 4–1 | Azam |
Source: RSSSF[9]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Simba edge Namungo to clinch Tanzania Community Shield". CAFOnline.com (kwa Kiingereza). CAF-Confedération Africaine du Football. Iliwekwa mnamo 2021-09-29.
- ↑ "Yanga beat Simba to lift the Community Shield". The Citizen (kwa Kiingereza). 2021-09-25. Iliwekwa mnamo 2021-09-29.
- ↑ "TFF Community Shield – TFF" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-09-29.
- ↑ "Tanzania Community Shield: Francis Kahata scores as Simba SC floor Azam FC". www.goal.com. Goal. Iliwekwa mnamo 2021-09-29.
- ↑ https://sokalabongo.com/2023/05/kuhusu-kubadili-mfumo-wa-ngao-ya-jamii-ukweli-huu-hapa-simba-na-yanga-bado-ziko.html
- ↑ https://spotileo.co.tz/ngao-ya-jamii-msimu-huu-itakuwa-na-msisimuko/
- ↑ https://trtafrika.com/sw/sports/simba-sc-bingwa-kombe-la-ngao-ya-jamii-2023-14470104
- ↑ "Simba SC clinched Community Shield title over Namungo FC". Africa Top Sports. 31 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 2 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Tanzania - List of Cup Winners". RSSSF. Iliwekwa mnamo 2021-09-30.