Hoteli ya Kibo Peak Palace

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hoteli ya Kibo Peak Palace ni hoteli ya fahari nchini Tanzania iliyopo Morogoro Mjini kwenye barabara Kuu kuelekea Mkoa wa Dar es Salaam, kilomita moja kutokea Stendi Kuu ya mabasi Msamvu katika Mkoa wa Morogoro.[1]

Pia hoteli hii hushiriki mambo mbalimbali ya kijamii na shughuli za uhamasishaji ndani ya Mkoa wa Morogoro kupitia Makundi mbalimbali katika kuinua Uchumi na uwekezaji.[2]

Matukio[hariri | hariri chanzo]

Bustani ya Hoteli ya Kibo Peak Palace, Morogoro Mjini

Hoteli hii inamilikiwa katika mfumo wa sekta binafsi na inashiriki mara kwa mara kutoa huduma kwa wasafiri na wanajamii wengine wanaotumia barabara ya Morogoro-Dar es Salaam kwa usafiri wa kila siku pamoja na vituo vingine vya biashara.[3]

Mkoa wa Morogoro kwa miongo tofauti Wadau wa ndani huandaa mashindano ya sanaa na kusaka vipaji ndani ya mkoa, pia hoteli ya Kibo Peak imeweza kuchangia na kushiriki shughuli hizo kama mdau.[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons