Nenda kwa yaliyomo

Hospitali ya Itete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hospitali ya Kilutheri ya Itete inapatikana katika mkoa wa Mbeya na inamilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania dayosisi ya Konde.

Hospitali hii ilifunguliwa mwaka 1963. Itete Lutherani Hospitali inapatikana katika wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya nchini Tanzania. Hospitali ya Itete ina jumla ya vitanda 120, na inahudumia watu wapatao 42,991. Inapata misaada kutoka serikalini kwa ajili ya vitanda 66 na wafanyakazi. [1]