Nenda kwa yaliyomo

Nyoka-misitu Njano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Hormonotus modestus)
Nyoka-misitu njano

Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Familia: Lamprophiidae (Nyoka walio na mnasaba na chata)
Oppel, 1811
Nusufamilia: Lamprophiinae
Oppel, 1811
Jenasi: Hormonotus
Hallowell, 1857
Spishi: H. modestus (A.M.C. Duméril, Bibron & A.H.A. Duméril 1854

Nyoka-misitu njano (Hormonotus modestus) ni nyoka wa familia Lamprophiidae ambao wanatokea misituni kwa Afrika ya Magharibi na ya Mashariki. Kuna spishi nyingine za nyoka-misitu katika jenasi Buhoma.

Nyoka huyu ni mrefu kiasi, hadi sm 90 lakini sm 40-70 kwa kawaida. Kichwa chake kina umbo wa pea. Rangi yake ni njano, hudhurungi au kahawiakijivu. Magamba ya kichwa yana kingo nyeupe.

Nyoka-misitu njano hukiakia usiku na hupumzika mchana chini ya majani makavu au katika vishimo. Hula wagugunaji na mijusi.

Nyoka huyu hana sumu na anaweza kukamatwa bila shida kwa sababu hawang'ati kwa kawaida.

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyoka-misitu Njano kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.