Halima Ali Adan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Halima Ali Adan
Picha ya Halima Adan
Picha ya Halima Adan
Nchi Tanzania
Kazi yake Mwanaharakati

Halima Ali Adan ni Msomali mwanaharakati wa haki za kijinsia, na mtaalamu wa ukeketaji. Ni mwenyekiti mwenza wa kikosi kazi cha ukatili wa kijinsia na meneja wa programu Okoa Watoto na Wanawanake wa Somalia.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Adan alizaliwa na kukulia Mombasa, Kenya.[1] Alisomea sayansi ya kompyuta chuo kikuu cha Greenwich huko London ambapo alipata shahada yake ya kwanza. Baada ya kupata shahada ya pili ya mafunzo ya maendeleo, Adan alianza kufanyia kazi katika shirika la kutoa huduma za intaneti Kenya.[1][2]

Shughuli[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka 2014, Adan aliajiriwa na shirika la Save Somali Women and Children (SSWC) kama meneja wa program na mwenyekiti mwenza wa kikosi kazi cha ukatili wa kijinsia.[3] SSWC ilianzishwa mwaka 1992 Mogadishu na mwanamke wa kisomali, ambaye lengo lake kutengeneza shirika lisilo la kibiashara ambalo litaunga mkono wanawake na wasichana wa Kisomali ambao wamepitia uzoefu wa kikatili na umaskini katika jamii zao.[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "International Women's Day: Giving more assistance to the vulnerable community in Somalia for the last 2 years.". gov.UK. Iliwekwa mnamo 24 July 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Halima Adan". Peace Builders.org. Iliwekwa mnamo 24 July 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "Dialogue for Action on Aid Localisation in Somalia". Humanitarian Leadership Academy. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-07-21. Iliwekwa mnamo 24 July 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. "Who is SSWC?". Save Somali Women and Children. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-25. Iliwekwa mnamo 24 July 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Halima Ali Adan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.