Geneviève Waïte

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Geneviève Waïte

Geneviève Waïte (13 Februari 1948 - 18 Mei 2019) alikuwa mwigizaji, mwimbaji na mwanamitindo wa Afrika Kusini.[1]. Umaarufu wake wa uigizaji alikuwa mhusika mkuu katika filamu ya mwaka 1968 iliyofahamika kwa jina la Joanna.[2].Kama mwanamitindo, alipigwa picha ya Vogue magazine mnamo mwaka 1971 na Richard Avedon.[2] Na, mnamo mwaka 1974, alirekodi albamu yake ya pekee kama mwimbaji.[2]

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Waïte aliolewa mara ya kwanza na Matthew Reich mnamo 10 Desemba 1968.[3]Baadaye, Waïte aliolewa na mwanamuziki John Phillips mnamo tarehe 31 Januari 1972.[2].Walikuwa na watoto wawili, waigizaji Tamerlane Phillips amezaliwa mwaka 1971 na Bijou Phillips amezaliwa mwaka 1980.[2] Waliachana mnamo mwaka 1985.Baadaye aliolewa na Norman Buntaine na baadaye walitengana.[3][4]

Muziki[hariri | hariri chanzo]

Albamu ya Waïte ya mwaka 1974 Romance is on the Rise ilitengenezwa na mumewe wa pili John Phillips,zamani wa kikundi cha folk rock the Mamas & the Papas.Toleo la mwaka 2011 la albamu kwenye CD linamjumuisha toleo la Jalada ya wimbo wa Velvet Underground.[5]

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 18 Mei 2019, Waïte alikufa katika usingizi wake huko Los Angeles, California. Binti yake, Bijou, alitangaza kifo hicho siku kadhaa baadaye.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Geneviève Waïte. allmovie.com. Iliwekwa mnamo 17 January 2010.
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 "Geneviève Waïte, 71, Star of the Swinging-’60s Film ‘Joanna,’ Dies", The New York Times, The New York Times Company, 24 May 2019. Retrieved on 19 September 2020. 
  3. 3.0 3.1 Geneviève Waïte. Iliwekwa mnamo 19 September 2020.
  4. american female singer songwriters. Air Structures (August 2004). Jalada kutoka ya awali juu ya 4 October 2009.
  5. Genevieve Waite. Amazon (company). Iliwekwa mnamo 19 September 2020.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Geneviève Waïte kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.