Galvanometa
Galvanometa ni kifaa kilichotengenezwa kimakanika na kiumeme chenye uwezo wa kuhisi/kugundua na kupima mkondo wa umeme.
Mara nyingi Galvanometa ni kifaa cha kianalojia ambacho hutumika kama ameta kupimia mawimbi ya umeme katika sakiti ya umeme kwa kutumia kizio kiitwacho ampea.
Galvonometa hupima mkondo wa umeme kwa kutumia mshale ambao huonesha kiasi cha mkondo wa umeme kipitacho katika sakiti.
Jina linatokana na Luigi Galvani, mwanafizikia wa Italia.