Fundi Konde

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Fundi Konde (24 Agosti 192429 Juni 2000) alikuwa mwanamuziki kutoka nchini Kenya. Fundi Konde ni mmoja kati ya watumbuizaji wa mwanzo kabisa nchini Kenya, na husemekana yeye ndiye mwanamuziki wa kwanza kucharaza gitaa la umeme huko Afrika Mashariki. Alipiga na kutunga muziki wake kwa Kiswahili huku akichanganya mahadhi ya Rumba la Kiafrika.

Kazi ya uanamuziki ilianza nyakati zile za Vita Kuu ya Pili ya Dunia, wakati huo alikuwa akiwatumbuizia vikosi vya kutoka Afrika Mashariki akiwa jeshini huko Asia Kusini. Alivyorudi nyumbani Kenya, akatatengeneza rekodi za awali ikiwa pamoja na "Mama Sowera", "Majengo Siendi Tena", "Kipenzi Waniua Ua" na "Jambo Sigara". Aliendelea kutumbuiza na kutoa santuri nyengine mpaka 1963 alipostaafu hadi hapo mwanzoni mwa miaka ya 1980 alipoanza tena kuimba, kutunga na kutayarisha.

Mwanamuziki huyu alizaliwa mnamo 1924 katika kijiji cha Mwabayanyundo, Wilaya ya Kilifi. Anatoka katika kabila la Wagiriama. Fundi Konde alifariki mnamo mwaka wa 2000 huko nyumbani kwake Kibera, Nairobi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fundi Konde kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.