Fumbo
Mandhari
Fumbo (kutoka kitenzi "kufumba"; kwa Kiingereza "mystery", kutoka neno la Kigiriki μυστήριον, myusterion, ambalo mzizi wake ni μύω, myuo, "nanyamaza") ni jambo ambalo linanyamazisha watu kwa jinsi linavyozidi uwezo wa akili yao kuelewa.
Mbele ya fumbo, kila mmoja anaweza kulikubali kwa imani au kulikataa. Hoja haziwezi kutosha kumfanya aamue la kwanza au la pili.
Hata hivyo, baada ya kuamini, pengine mtu anaweza kutumia akili na hoja ili kujaribu kuelewa na kueleza kwa kiasi fulani fumbo lenyewe, mradi kwanza amelikubali kama limefunuliwa na Mungu.
Ufafanuzi huo unategemea hasa maandiko matakatifu ya dini husika, kwa mfano Biblia kwa Wakristo.
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |