Frances M. Beal
Mandhari
Frances M. Beal, pia anajulikana kama Fran Beal, (alizaliwa Januari 13, 1940, huko Binghamton, New York) ni mwanaharakati wa haki za wanawake na amani..[1] Lengo lake limekuwa zaidi kuhusu haki za wanawake, haki ya rangi, kazi ya kupinga vita na amani, pamoja na mshikamano wa kimataifa.
Beal alikuwa mwanachama mwanzilishi wa SNCC kamati ya ukombozi ya wanawake weusi, ambayo baadaye ilibadilika na kuwa Third World Women's Alliance.[2] Anajulikana sana kwa chapisho lake, lililoitwa “Double Jeopardy: To Be Black and Female", linalotoa nadharia ya makutano ya ukandamizaji kati ya rangi, tabaka, na jinsia. Beal kwa sasa anaishi Oakland, California.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Cengage Learning". Accessmylibrary.com. Iliwekwa mnamo 2015-10-16.
- ↑ Hartmann, Maureen. "Frances Beal: A Voice for Peace, Racial Justice and the Rights of Women". The Street Spirit.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Frances M. Beal kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |