Fran Hosken
Fran P. Hosken (Vienna, Austria, 1920 - 2 Februari 2006) alikuwa mbunifu, mwandishi, na mwanaharakati wa masuala ya kijamii wa Marekani. Alianzisha Women International Network mwaka 1975, na kuchapisha robo ya jarida la masuala ya afya ya wanawake ambalo baadae lilijulikana katika tafiti za ukeketaji wa wanawake.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Hosken alizaliwa kama Franziska Porges huko Vienna, ambapo baba yake Otto Porges alikuwa tabibu kutoka Bohemia (Brandys nad Labem, Czech Republic),[1] na alihamia na familia yake nchini Marekani mwaka 1938na kusoma katika chuo cha Smith, na mwaka 1944 alipata shahada ya uzamivu kutoka shule ya ubunifu Harvard, ni mwanamke wa kwanza kufanya hivyo. Alijiunga kulinda pwani wakati wa vita ya pili ya dunia, kufanya kazi katika mawasiliano. Alioana na James Hosken mwaka 1947, na walianzisha Kampuni ya Hosken mwaka 1947. Walikuwa na watoto watatu, na waliachana mwaka 1962.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Hosken alianzisha kampuni ya Hosken na mumewe James Hosken mwaka 1947. Moja ya mradi wake wakwanza, zana zenye rangi nyingi, akawa mwenye mafanikio kibiashara. Kazi zake zilisambazwa na Knoll, Ramornna Macy na kuonyeshwa kwenye soko la bidhaa Chikago na Milan Triennale. Licha ya kufanikiwa mapema, Kampuni ilifungwa mwaka 1951.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ http://www.whonamedit.com/doctor.cfm/581.html
- ↑ "The Lives They Lived: Fran Hosken". WEINBERG MODERN (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-03-17.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fran Hosken kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |