Nenda kwa yaliyomo

Fibonacci

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fibonacci

Fibonacci (mnamo 1175 - 1250) alikuwa mtaalamu wa hisabati kutoka nchini Italia. Anakumbukwa kama mwanahisabati muhimu zaidi wa Ulaya wakati ya zama za kati.

Jina lake la kiraia ilikuwa Leonardo wa Pisa lakini aliitwa kwa jina la baba yake Bonacci.

Mfululizo wa Fibonacci[hariri | hariri chanzo]

Fibonacci anakumbukwa hasa kwa jedwali la namba linaloitwa mfululizo wa Fibonacci.

Linaanza hivi: 1, 1, 2, 3, 5, 8, 13, 21, 34, 55, 89, ...

Katika mfululizo huu namba inayofuata ni jumla ya namba mbili zinazotangulia:

1 + 1 = 2
  1 + 2 = 3
    2 + 3 = 5
      3 + 5 = 8
        5 + 8 = 13
          8 + 13 = 21
            13 + 21 = 34
               21 + 34 = 55
                 34 + 55 = 89
                    55 + 89 = 144
                      89 + 144 = 233
                         144 + 233 = 377
                            233 + 377 = 610
                               377 + 610 = 987
                                  610 + 987 = 1597
                                     987 + 1597 = 2584
                                     na kadhalika...