Nenda kwa yaliyomo

Federico Moura

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Federico José Moura (23 Oktoba 1951 - 21 Desemba 1988) alikuwa mwimbaji wa Argentina, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa muziki, mbunifu wa mavazi na kiongozi wa bendi ya New wave, iliyoundwa na kaka zake Julio na Marcelo mnamo mwaka 1981. Moura alichukuliwa kama mmoja wa wanamuziki wenye ushawishi mkubwa nchini Hispania kutokana na aina yake ya muziki wa Rock alioufanya.[1][2]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Federico José Moura alizaliwa mnamo 23 Oktoba mwaka 1951 huko Berisso, kitongoji cha Greater La Plata huko Mkoa wa Buenos Aires, nchini Argentina. Baba yake alikuwa Pico Moura aliyekuwa mwanasheria, na mama yake aliitwa Velia Oliva, aliekuwa mwalimu wa shule na mpiga piano.[3] Alikuwa wa mwisho kati ya kaka zake wanne; kaka yake mkubwa, Jorge, alikuwa mwanachama hai wa jeshi la Wananchi la Mapinduzi (ERP), na alitekwa nyara na kupotea mnamo mwaka 1977 na jeshi la kidikteta la mwisho nchini Argentina mwaka (1976-1983).[4][5]

Federico alionyesha kupendezwa na muziki tangu akiwa na umri mdogo, akaanza kupiga gitaa na kinanda akiwa na umri wa miaka minne. Alimaliza shule ya upili katika Colegio Nacional de La Plata akajiunga na Chuo Kikuu cha La Plata.[4] , kama kaka zake wakubwa, katika umri wake wa ujana alifanya mazoezi ya mchezo wa Rugby akiwa na ya klabu ya La Plata Rugby Club.[5]

Kazi ya muziki

[hariri | hariri chanzo]

Katika miaka yake ya ujana, Moura alikuwa mpiga bass katika kundi la Dulcemembriyo, kundi ambalo lilifanya ziara katika maeneo ya Amerika ya Kilatini. Kisha baade alianzisha makundi mawili ya mzuki ambayo ni Las Violetas pamoja na Marabunta.[3] Kuelekea mwisho wa miaka ya 1970, Moura aliandikishwa na kaka zake Julio na Marcelo kuwa kiongozi wa sauti wa bendi yao ya Duro; Julio alikuwa akipiga gita na kaka yake Marcelo alikuwa mpiga kinanda, Enrique Muguetti alikuwa akipiga bezi (bass), Ricardo alikuwa mpiga gitaa la pili na Mario Serra alikuwa akipiga ngoma.[6]

Virusi mnamo mwaka 1985 (na Moura akiwa mbele na katikati).

Kikundi kilianza kujulikana kwa jina la "Virus" mnamo mwaka 1981. Mnamo Januari mwaka huo, bendi hiyo ilikuwa na gig yao ya kwanza katika Asociación Universal huko La Plata.[3] Mnamo Septemba mwaka 1981, Bendi ya Virus ilifanya maonyesho yao ya kwanza Ezeiza Buenos Aires, na wiki moja baadaye, walianza kurekodi katika studio ya muziki ya CBS Records.

Katikati ya mwezi Oktoba mwaka 1988, Moura alilazwa katika hospitali ya CEMIC huko Recoleta, Buenos Aires. Alifariki dunia mnamo Desemba 21 mwaka huo huo, katika eneo la San Telmo katika mji wa Buenos Aires, kutokana na matatizo katika njia ya upumuaji; alikuwa na uzani wa kilo 35. Alikuwa ameongozana na mama yake Velia.[3] Alizikwa katika makaburi ya La Chacarita. Mnamo mwaka 2004, mabaki ya Federico yalifukuliwa na kaka zake Marcelo na Julio, kisha kuchomwa moto na majivu ya mwili wake yalitupwa katika mto Río de la Plata.[7]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
  1. "Federico Moura: no lo vimos caminar porque siempre volaba". Ministerio de Cultura (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 27 Januari 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Se cumplen 32 años sin Federico Moura". Filo.news (kwa Kihispania). 20 Desemba 2020. Iliwekwa mnamo 27 Januari 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 Jalil, Oscar (29 Septemba 2017). "El legado de belleza, lucha y redención de Federico Moura". Rolling Stone (kwa Kihispania). La Nación. Iliwekwa mnamo 27 Januari 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 Zabiuk, Mariel G. (11 January 2009). "Territorios del rock. Jóvenes universitarios y cambios culturales, 1960-1970". Los Trabajos y Los Días (kwa Kihispania). 1. National University of La Plata: 69–87. ISSN 1852-7280. Iliwekwa mnamo 27 January 2021. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help)
  5. 5.0 5.1 Anguita, Eduardo; Cecchini, Daniel (5 Januari 2020). "La historia de Jorge Moura, el hermano guerrillero de los músicos de Virus desaparecido por la dictadura". Infobae (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 27 Januari 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Garrido, Mónica (21 Desemba 2018). "Federico Moura: la inmortal voz de Virus en cinco de sus canciones". La Tercera (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 27 Januari 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Chiappero, Fabiana (21 Desemba 2020). "32 años sin Federico Moura: imágenes paganas de carisma, talento y sexualidad". Aires de Santa Fe (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 27 Januari 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Federico Moura kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.