Fatima Trotta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Fatima Trotta
Amezaliwa2 Julai 1986
UtaifaItalia
Kazi yakeMchekeshaji

Fatima Trotta (alizaliwa Naples, 2 Julai 1986) ni mwigizaji wa kike, pia ni mchekeshaji na mtangazaji wa runinga nchini Italia.[1]

Maisha yake na kipaji chake[hariri | hariri chanzo]

Akiwa mtoto alishiriki katika mashindano kadhaa ya Urembo, akiwa na umri mdogo alifanya kazi kwenye televisheni ya Neopolitan katika kipindi kilichokuwa kinaongozwa na Maria Teresa Ruta.[2]

Baada ya kuonekana kwenye onyesho la vipaji liitwalo Rai 1 talent show I Raccomandati mnamo 2005, alifanikiwa kuonyesha kipaji chake cha uigizaji kwenye tamthilia iliyoonyeshwa kwenye televisheni ya Rai 3 Un Posto al Sole.[3]

Tangu mwaka 2009 Fatima Trotta ni mtangazaji wa maudhui tofautitofauti Made in Sud, alitangaza kwa mara ya kwanza kwenye Comedy Central na baadaye alitangaza kwenye chaneli ya televisheni ya Rai 2.[2][4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fatima Trotta kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.