Fabián Ruiz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fabian akiwa uwanjani.

Fabián Ruiz Peña (anajulikana kama Fabián; alizaliwa 3 Aprili 1996) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Hispania anayechezea Klabu ya Italia S.S.C. Napoli na timu ya taifa ya Hispania. Tangu Juni 2019, Fabian pia ni mchezaji wa kikosi cha kwanza cha Hispania.

Yeye kama kiungo wa kati anayetumia mguu wa kushoto, Fabian anajulikana kwa maono yake ya pasi, nguvu, udhibiti wa mpira, na anaweza kucheza katika mifumo mbalimbali, kama vile 4-5-2, 4–3-3, na 4-2-1-1.

Alizaliwa Los Palacios, Seville huko Hispania. Fabián alijiunga na kikosi cha vijana cha Real Betis mnamo 2004, akiwa na umri wa miaka minane.

Mnamo 5 Julai 2018, Fabián alijiunga na S.S.C. Napoli kwa mkataba wa miaka mitano hadi 2023 Imeripotiwa kuwa ada yake ilikuwa milioni 30. Alicheza mchezo wa kwanza mnamo tarehe 16 Septemba katika mchezo wa ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Red Star Belgrade, akicheza dakika 90 bila ya goli lolote.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fabián Ruiz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.