Sundakuwili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Eryx)
Sundakuwili
Sundakuwili mashariki (Eryx colubrinus)
Sundakuwili mashariki (Eryx colubrinus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Oda ya chini: Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
Familia: Boidae (Nyoka walio na mnasaba na kipiri)
Gray, 1825
Nusufamilia: Erycinae
Bonaparte, 1831
Jenasi: Eryx
Daudin, 1803
Ngazi za chini

Spishi 12:

Sundakuwili ni spishi za nyoka wa jenasi Eryx katika familia Boidae. Wamepewa jina hili kwa sababu ncha zote mbili zinaonekana sawa.

Nyoka hawa ni wafupi. Spishi ndefu kabisa (E. conicus) inaweza kufika mita moja, lakini spishi fupi hufika sm 40 tu. Kichwa kina umbo wa risasi bila shingo na wenye macho madogo. Mkia ni mfupi, chini ya 10% ya urefu mzima. Kwa kawaida wana mabaka kahawia au meusi juu ya msingi wa rangi nyepesi kama kijivu, njano au machungwa, lakini kuna namna zilizo na rangi moja kama nyekundu, kahawia, hudhurungi au kijivu.

Sundakuwili hujificha chini ya mchanga au hukaa katika vishimo vya wanyama au chini ya mawe. Mawindo yakija karibu nyoka hushambulia kwa kasi kubwa. Mawindo ni wagugunaji na ndege wadogo, mijusi na nyoka wengine wadogo. Spishi nyingine huwinda mchana, nyingine usiku.

Kama chatu nyoka hawa hawana sumu na huua mawindo kwa ubinyaji. Huzongomeza mwili wao kuzunguka kidari cha mawindo kisha kubana kwa nguvu ili kuzuia mawindo asipumue mpaka akufe. Halafu humwakia mzima.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za Asia na Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sundakuwili kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.