Nenda kwa yaliyomo

Erik Lamela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lamela akiwa Tottenham Hotspurs.

Erik Manuel Lamela (alizaliwa 4 Machi, 1992) ni mchezaji wa soka wa Argentina ambaye anacheza kama kiungo mshashambulia au winga kwa klabu ya Tottenham Hotspurs na timu ya taifa ya Argentina.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa huko Buenos Aires nchini Argentina. Alianza kazi yake katika klabu ya River Plate , mwaka 2011 alihamia AS Roma ya Italia kwa ada £ milioni 12. Baada ya misimu miwili ya Serie A kupita alijiunga na Tottenham kwa ada ya £ milioni 25.8 .

Kimataifa tangu mwaka 2011, alikuwa sehemu ya kikosi cha Argentina ambacho kilicheza kombe la dunia 2014,copa america 2015 na kombe la dunia la 2018.


Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Erik Lamela kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.