Nenda kwa yaliyomo

Erich Honecker

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Erich Honecker


Katibu Mkuu wa Chama cha Maungano cha Kisoshalisti cha Ujerumani
mtangulizi Walter Ulbricht
aliyemfuata Egon Krenz

Mwenyekiti wa Baraza la Dola
mtangulizi Willi Stoph
aliyemfuata Egon Krenz

tarehe ya kuzaliwa (1912-08-25)25 Agosti 1912
Neunkirchen, Germany
tarehe ya kufa 29 Mei 1994 (umri 81)
Santiago, Chile
utaifa German
chama Chama cha Muungano Kisoshalisti Ujerumani
ndoa Edith Baumann
Margot Feist (1953-1994)
Fani yake Mwanasiasa

Erich Honecker (25 Agosti 1912 - 29 Mei 1994) alikuwa mwanasiasa wa Kikomunisti wa Ujerumani Mashariki ambaye aliongoza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani kutoka mwaka 1971 hadi 1989.

Baada ya maungano ya Ujerumani ya 1990, alihamia Umoja wa Kisovyeti lakini alirudishwa Ujerumani na serikali mpya ya Urusi, ambapo alifungwa na kuhukumiwa kwa uhaini na uhalifu uliotekelezwa wakati wa vita baridi. Walakini, wakati alikuwa mgonjwa wa saratani ya ini, aliachiliwa kutoka gerezani. Alikwenda uhamishoni nchini Chile alipofariki mwaka 1994.

Asili na vyanzo vya kazi ya kisiasa

[hariri | hariri chanzo]

Honecker alizaliwa huko Neunkirchen, leo kwenye jimbo la Saarland, Ujerumani. Alikuwa na kaka wawili na dada watatu.

Alijiunga mnamo 1926 na Umoja wa Vijana wa Kikomunisti wa Ujerumani (KJVD) uliokuwa tawi la Chama cha Kikomunisti cha Ujerumani (KPD), na kuwa mwanachama kamili mwaka 1929. Kati ya 1928 na 1930 alifanya kazi kama fundi wa kuezeka paa. Baadaye alipelekwa Moscow kusoma katika Shule ya Kimataifa ya Lenin na kwa maisha yake yote aliendelea kama mwanasiasa wa kikazi.

Alirudi Ujerumani mnamo 1931. Baada ya Chama cha NSDAP cha Hitler kuchukua serikali, Wakomunisti walipigwa marufuku katiia Ujerumani, lakini eneo la Saar likikuwa na hali ya pekee kwa miaka miwili. Hadi 1935 Honecker alipinga jitihada za kuunganisha Saar na Ujerumani; hatimaye alikamatwa mnamo 1935 baada ya Wanazi kuingia madarakani pia Saar. Mnamo 1937, alihukumiwa miaka kumi kwa kazi yake ya kisiasa alikaa kifungoni hadi mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia . Baada ya gereza la Honecker kuvamiwa na kifaru cha Kirusi, alipata uhuru wake. Alibaki katika sehemu ya Ujerumani iliyokuwa chini ya mamlaka ya Jeshi Jekundu akajiunga tena na Wakomunisti wenzake akafaulu kupokelewa na kundi la Walter Ulbricht, Wakomunisti Wajerumani waliorudi pamoja na washindi Warusi.

Mwaka 1946 Honecker aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya chama na pia kuwa kiongozi wa Vijana Huru wa Kijerumani (FDJ), umoja wa vijana wote katika ukanda wa mamalaka ya Kirusi wa Ujerumani. Wakati mamlaka ya kijeshi ya Kirusi ililazimisha maungano ya vyama vya Kikomunisti na Kijamii-kidemokrasia (social democrat), Honecker alikuwa mwanahama wa Chama cha Muungano Kisoshalisti Ujerumani (SED).

Honceker alikuwa mbunge wa bunge katika eneo chini ya mamlaka ya Kisovyeti tangu uchaguzi wa Oktoba 1946. Baada ya kuundwa kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani kwenye Oktoba 1949, Honecker aliteuliwa kuingia katika Kamati Kuu ya chama mnamo 1950, alipokuwa mjumbe kamili mnamo 1958. Akiwa mwenyekiti wa umoja wa Vijana FDJ, alijitahidi hasa kupunguza athira ya vikundi vya vijana vya makanisa alivyotazama kama wapinzani wake wa kiitikadi. 1955 hadi 1957 Hoecker alikaa Moscow kwa masomo ya kiitikadi, na hapo alishiriki kwenye Mkutano wa XX wa Chama cha Kikomunisti ambako Nikita Krushchov alibomoa kumbukumbu ya Joseph Stalin.

Baada ya kurudi Berlin, alikuwa mjumbe kamili wa kamatu kuu akawajibika katika mambo ya usalama na kijeshi. Akiwa Katibu wa Usalama wa SED alisimamia ujenzi wa Ukuta wa Berlin kwenye mwaka 1961.

Kiongozi wa Ujerumani Mashariki

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 1971, Honecker alianza mapambano ya nguvu ya kisiasa dhidi ya mkuuwa Chama cha kikomunisti Walter Ulbricht. Kwa msaada wa serikali ya Kisovyeti alimlazimisha Ulbricht kujiuzulu akawa kiongozi mpya, au Katibu Mkuu, wa Chama cha SED. Tangu 1976 alikuwa pia Mwenyekiti wa Baraza la Dola na hivyo mkuu wa dola.

Honecker alijitahidi kuboresha maisha ya wananchi wake na Ujerumani ya Mashariki ilipata hali ya juu ya maisha katika nchi zote za Umoja wa nchi za kikomunisti. Hata hivyo, uwezo wa uchumi wa kisoshalisti uliendelea kubaki nyuma ya maendeleo katika magharibi ya Ujerumani kwenye Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani. Honecker alikazia utawala wa kisiasa katika himaya yake, alikandamiza upinzani wowote na kuimarisha mpaka ndani ya Ujeruamni ambako mamia waliuawa walipojaribu kutoroka kutoka mashariki kwenda magharibi. Kwa msaada wa mikopo kutoka magharibi Honecker aliweza kudumisha serikali yake. 1987 Honecker alitembelea Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kama mgeni rasmi wa chanselaa Kohl.

Mwishoni mwa miaka ya 1980 kiongozi wa Umoja wa Kisovyeti, Mikhail Gorbachov alibadilisha siasa ya ukomunisti kwa mitindo ya glasnost na perestroika, kama mageuzi ya kukomboa ukomunisti. Honecker, hata hivyo, alikataa kutekeleza mageuzi kama hayo katika GDR. Wakati harakati ya mageuzi ikienea kote Ulaya ya Kati na Mashariki kulikuwa na maandamano dhidi ya serikali ya Ujerumani Mashariki. Kubwa zaidi yalikuwa maandamano ya Jumatatu mnamo 1989 katika jiji la Leipzig . Viongozi wengine wa DDR waliamua kumwondoa Honecker, na kumlazimisha ajiuzulu mnamo 18 Oktoba 1989. Egon Krenz alichukua nafasi yake.

Baada ya kupinduliwa, Honecker alibaki bila nyumba wala makazi. Kwa muda wa miezi miwili alipata kimbilio katika nyumba ya mchungaji mmoja wa Kilutheri, baadaye alipelekwa katika hospitali ya kijeshi ya Kirusi pale Berlin. Madaktari walitambua kansa ya ini kwake. Kutoka hodspitali alipelekwa Moscow pamoja na mkewe, ili kuepuka mashtaka juu ya uhalifu wa Vita Baridi, hasa maagizo yake ya kzuia watu walioelekea magharibi hata kwa kutumia silaha. Baada ya Umoja wa Kisovyeti kuvunjika ma ,wisho wa ukomunisti pale, mnamo Desemba 1991, Honecker alikwenda kwa ubalozi wa Chile huko Moscow, lakini alirudishwa na serikali ya Boris Yeltsin mnamo 1992.

Honecher alikamatwa na kushtakiwa; lakini aliachiliwa kwa sababu ya afya mbaya na mnamo 13 Januari mwaka huo alihamia Chile kuishi na binti yake Sonja aliyeolewa na Mchile.

Alikufa kwa saratani ya ini huko Santiago, Chile mnamo 29 Mei 1994.

  • Honeker, Erich (1984). "Erich Honecker Speech on Peace (1984)". calvin.edu. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-08-16. Iliwekwa mnamo 17 Desemba 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: