Emmanuel Ake

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Emmanuel Ake
Youth career
Black Panther
Coast Stars
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
2000–2004AB45(3)
2004–2008Nordsjælland14(0)
2006Ølstykke (loan)15(1)
2006–2007Holbæk B&I (loan)22(9)
2007–2008HIK (loan)41(25)
2008–2009Herfølge23(17)
2009–2010HB Køge13(5)
2010–2011Lyngby Boldklub1(0)
2011Næstved Boldklub10(4)
2012Svebølle B&I0(0)
2012–FC Djursland0(0)
Timu ya Taifa ya Kandanda
2004–Kenya8(1)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 3 November 2011 (UTC).

† Appearances (Goals).

‡ National team caps and goals correct as of 3 November 2011 (UTC)

Emmanuel Ake Richard Muttendango (zamani alikuwa anajulikana kama Ali Akida; alizaliwa Mombasa, 11 Juni 1980) ni mwanakandanda mshambuliaji wa kimataifa kutoka Kenya ambaye katika misimu minane iliyopita amekuwa akizichezea vilabu tofauti nchini nchini Denmark.

Jina na tarehe ya kuzaliwa za uongo[hariri | hariri chanzo]

Wakati Ake alienda nchini Denmark kwa mara ya kwanza mwaka wa 2000, alijitambulisha kama Ali Rajab Akida, au Ali Akida, tu huku akisema kuwa alizaliwa mnamo 20 Desemba 1982. Baadaye ilikuja kugunduliwa kwamba taarifa hii ilikuwa si sahihi na kwamba jina lake halisi lilikuwa Emmanuel Ake Richard Muttendango, aliyezaliwa mnamo 11 Juni 1980. Ake hatimaye alipigwa faini ya DKK(pesa za Denmark) 7,000 na Mahakama ya mji mkuu wa Gladsaxe. Baada ya idadi ya maamuzi na rufaa kutoka pande zote husika, Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki na Shirikisho la Michezo la Denmark lilimpiga marufuku kwa muda wa miezi 3. Klabu ya Ake wakati huo, Akademisk Boldklub, pia ilipigwa faini ya 50,000 DKK na alama zote za timu ya kwanza na timu hifadhi za AB zilizokusanywa katika mechi ambazo Ake alishiriki, ziliondolewa.

Katika vilabu[hariri | hariri chanzo]

Nchini Kenya[hariri | hariri chanzo]

Babake anatoka Kenya, lakini mamake anatoka katika kisiwa ya Ushelisheli. Alianza wasifu wake kuu na klabu ya Black Panther, ambayo ilicheza katika ligi ya Mkoa wa Pwani (kiwango cha 3 nchini Kenya). Kisha alihamia klabu ya Coast Stars ambayo ina makao yake katika mji mkuu wa Mombasa na wakati alikua anacheza katika Ligi Kuu ya Kenya kabla ya kuhamia Denmark

Nchini Denmark[hariri | hariri chanzo]

Akiwa bado na umri mdogo wa miaka 20, Ake alitia saini mkataba wa klabu ya Akademisk Boldklub ambayo aliichezea kwa muda wa misimu minne - 2000/01, 2001/02, 2002/03 na 2003/04. Kisha aliamua kuhamia klabu ya FC Nordsjælland kwa misimu mingine miwili - 2004/05 na 2005/06.

Ake alipeanwa kama mkopo na klabu yake ya FC Nordsjælland kwa nusu ya pili ya msimu wa 2005/06 kwa klabu ya Ølstykke FC. Alikuwa mfungaji bora wa mabao wa klabu hiyo msimu huo ulipokamilika akiwa na mabao 14. Msimu uliyofuata, Ake alipeanwa tena kama mkopo katika klabu ya divisheni ya pili ya Holbæk B&I ambapo pia alikamilisha msimu huo kama mfungaji bora wa mabao wa klabu hiyo akiwa na mabao ya 11.

Katika msimu wa 2007/08, Ake alipeanwa tena kama mkopo lakini wakati huu katika klabu ya Divisheni ya Kwanza ya Hellerup IK (HIK). Kwa mara nyingine tena akawa mfungaji bora wa mabao katika klabu hiyo akiwa na mabao 13 lakini mabao yake hayakusaidia klabu hiyo kubaki katika divisheni hiyo kwani klabu hiyo iliangushwa hadi divisheni ya pili.

Kwa sasa Ake ni mchezaji wa klabu ya Herfølge BK baada ya kutia saini mkataba wa miaka mitatu. Alijiunga na klabu hiyo baada ya kutangazwa kama ajenti wa bure na klabu ya FC Nordsjælland.

Kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Ake alikuwa katika timu ya Kenya katika Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Tunisia mwaka wa 2004 na aliichezea mechi tatu Timu ya Taifa ya Kandanda ya Kenya, Harambee Stars. Alifunga bao la tatu wakati Kenya ilipata ushindi wake wa kwanza katika shindano hilo la Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Burkina Faso.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Emmanuel Ake kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.