Nenda kwa yaliyomo

Emeka Ojukwu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Emeka Ojukwu

Chukwuemeka Odumegwu Ojukwu (* 4 Novemba 1933 Zungeru (Nigeria) ni mwanasiasa wa Nigeria aliyekuwa mwanajeshi na rais wa jamhuri ya Biafra iliyojitenga na Nigeria 1967 - 1970.

Maisha yake

[hariri | hariri chanzo]

Ojukwu amezaliwa katika kabila la Waigbo. 1957 alijiunga na jeshi. 1966 akiwa kanali alikuwa afisa kiongozi na gavana wa kijeshi wa mkoa wa mashariki. Baada ya mauaji wa Waigbo wengi upande wa kaskazini ya Nigeria alitangaza uhuru wa mkoa wa mashariki penye Waigbo wengi ulioitwa "Biafra".

Ojukwu alikuwa rais wa Biafra kati ya 30 Mei 1967 na 8 Januari 1970. Baada ya Biafra kushindwa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Nigeria Ojukwu alikimbia Côte d'Ivoire. Mwaka 1980 alikaribishwa na rais wa Nigeria Alhaji Shehu Shagari arudi nyumbani.

Katika uchaguzi wa 1983 Ojukwu aligombea kiti cha bunge baadaye pia uraisi lakini hakuchaguliwa. Aligombea tena urais katika uchaguzi wa Aprili 2007 akafikia nafasi ya sita kwa kura 155,000. Alipinga uchaguzi akidai haukuwa sahihi.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]