Nenda kwa yaliyomo

Emanueli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kristo Emanueli, picha takatifu iliyofunikwa kwa fedha, kazi ya Simon Ushakov, 1668.

Emanueli (au (kwa Kiebrania: עִמָּנוּאֵל, Immanuel, yaani, "Mungu pamoja nasi") ni jina la Kiebrania lililotajwa na nabii Isaya (Isa 7:13-16) kama ishara ya kwamba Mungu atasimamia ukoo wa Daudi dhidi ya maadui.

Injili ya Mathayo (1:22–23) inataja maneno hayo kadiri ya tafsiri ya Kigiriki maarufu kwa jina la Septuaginta ambayo ilifafanua kwamba mwanamwali atakayemzaa huyo mtoto wa kiume ni bikira.

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Emanueli kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.