Elijah McCoy

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Elijah McCoy
Elijah McCoy

Elijah J. McCoy (Mei 2, 1844 - Oktoba 10, 1929) alikuwa Mmarekani mwenye asili ya Afrika ambaye ni mwanzilishi wa vilainishi ili kufanya treni kwenda vyema.

Alizaliwa huko Colchester, Ontario, akafa huko Detroit, Michigan.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Eliya J. McCoy alizaliwa huru mwaka 1843 au 1844 huko Colchester, Ontario, Canada kwa George na Mildred (Goins) McCoy. Walikuwa watumwa wakimbizi ambao waliokoka kutoka Kentucky kwenda Canada kupitia wasaidizi kwa njia ya reli ya chini ya ardhi.

George na Mildred waliwasili katika mji wa Colchester, Essex, Ontario, Canada mwaka 1837 kupitia Detroit. Elija McCoy alikuwa na ndugu kumi na moja. Watoto kumi walizaliwa huko Canada kutoka kwa Alfred (1839) hadi William (1859).

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Elijah McCoy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.