Edvige Carboni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Edvige Carboni (Pozzomaggiore, Sassari, 2 Mei 1880 - Roma, 17 Februari 1952) alikuwa mwanamke Mkristo wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko nchini Italia.

Tangu utotoni alijaliwa karama za pekee, zikiwemo njozi, kutoka nje ya nafsi na, akiwa na umri wa miaka 29, madonda matakatifu, pamoja na kuteswa na shetani.

Alitangazwa na Papa Fransisko kuwa mwenye heri tarehe 15 Juni 2019.