Nenda kwa yaliyomo

Dubni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Dubnium)


Dubni (dubnium)
Jina la Elementi Dubni (dubnium)
Alama Db
Namba atomia 105
Mfululizo safu Metali ya mpito
Uzani atomia 262.0
Valensi 2, 8, 18, 32, 32, 11, 2
Densiti 29.3 g/cm³ (kadirio)
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Asilimia za ganda la dunia 0 % (elementi sintetiki)
Hali maada inaaminiwa ni mango
Mengineyo tamburania, nururifu

Dubni (kwa Kiingereza: Dubnium) ni elementi sintetiki yenye namba atomia 105 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni takriban 262. Alama yake ni Db.

Baada ya kugunduliwa katika maabara iliitwa majina tofauti kama vile eka-tantalum, hahnium na unnilpentium lakini hatimaye jina likawa Dubni kwa kumbukumbu ya mji wa Urusi wa Dubna ambako iligunduliwa.

Ni elementi nururifu sana isiyopatikana kiasili. Ni elementi sintetiki au tamburania yaani haipatikani kiasili. Sababu yake ni kwamba nusumaisha ya isotopi zake ni fupi mno. 268Db (isotopi thabiti zaidi) ina nusumaisha ya masaa 28[1].

  1. https://newscenter.lbl.gov/2010/10/26/six-new-isotopes/ Six New Isotopes of the Superheavy Elements Discovered], tovuti ya Berkeley Lab ya October 26, 2010, iltazamiwa Januari 2020
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dubni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.