Donald "Flash" Gordon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Donald Gordon
Siku ya Kuzaliwa: 17 Julai 1920
Jina la utani: "Flash"
Pahali pa Kuzaliwa: Garland, Texas
Uzalendo: Marekani
Kikosi cha Jeshi: Wanamaji
Miaka ya Kazi: 1942 - 1967
Cheo: Kapteni
Vita aliyoshiriki: Vita ya Pili ya Dunia
Tuzo: Distinguished Flying Cross

Donald "Flash" Gordon (17 Julai 1920 - 4 Januari 2010) alikuwa rubani shujaa wa vita wa Marekani. Alipiga risasi zaidi ya ndege 7 za Ujapani katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Alikuwa rubani wa kivita wa Kikosi cha Wanamaji wa Marekani na alipokea tuzo ya Distinguished Flying Cross.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Donald alizaliwa Garland, Kansas tarehe 17 Julai 1920. Alisoma katika Shule ya Upili ya Fort Scott na kumaliza masomo yake ya kiwango hicho katika mwaka wa 1931.Akaendelea na masomo yake katika Chuo cha Fort Scott Junior College akimaliza katika mwaka wa 1941. Gordon alisoma ,pia, mafunzo ya urubani kwa raia na akapata leseni yake. Baada ya kumaliza chuo, Gordon aliingia mpango wa mafunzo ya Naval Aviation Cadet Program mnamo 7 Julai 1941. Alimaliza mafunzo yake na akaajiriwa kazi kama Ensign mnamo 12 Machi,1942, akiwa umri wa miaka 21. Kazi yake ya kwanza ilikuwa kama rubani wa kikundi cha Fighter Squadron 10 (VF-10). Kikundi hiki kiliitwa hapo baadaye Grim Reapers.

Katika mwezi wa Oktoba 1942, kikundi cha VF-10 kikabebwa na meli ya kivita,Enterprise. Ndege ya kwanza aliyoiendesha Gordon kutoka meli hiyo,Enterprise, ilikuwa ndege ya aina ya F4F Wildcat. Gordon alipata nafasi ya kuumiza adui wake mnamo 26 Oktoba katika Vita ya Santa Cruz. Gordon aliangusha ndege mbili ya aina ya Mitsubishi 97 kwa kutumia risasi na bomu. Katika rekodi zake waliongeza ndege moja ingine chini ya orodha ya "labda" kwa sababu vita ilikuwa kali na haingewezwa kuthibitishwa.

Alipata nafasi ingine mnamo 30 Januari 1943 katika ziara ya uchunguzi iliyohusisha ndege 12 ya Combat Air Patrol(CAP). Walikuwa wakizuru sehemu kaskazini mashariki ya meli, Gordon akawa wa kwanza kuona ndege 11 ya aina ya Mitsubishi G4M. Akawaarifu wenzake kuhusu adui aliowaona na wakashambulia adui waliokuwa wakiwapiga risasi pia. Gordon alishambulia ndege moja ya Ujapani. Ndege hiyo ikapata moto na kuanguka baharini. Kisha akageuza ndege yake na akaangusha ndege nyingine vivyo hivyo.

Gordon hakupata sifa aliyostahili kwa kuangusha ndege hizo mbili kwa sababu alikuwa wa mwisho kufika katika chumba maalum cha kupiga ripoti. Alipokuwa akifika chumba hicho na ripoti yake na madai yake ya ushindi, akagundua kuwa kulikuwa na madai 19 kwa ndege 11 za adui ingawa yeye alijua kuwa alipiga risasi mbili zikaanguka na mbili zikahepa.

Huu ulikuwa mwanzo mzuri sana katika kazi ya rubani huyu wa kivita. Baada ya kushiriki katika mapambano mawili tu na adui, Gordon alipewa jina la utani la "FLASH GORDON". Jina ambalo lilikuwa jina la shujaa wa kivita wa hekaya za kisayansi. Sifa hii ilistahili kwa sababu aliangusha ndege tatu zilizothibitishwa ,ndege mbili zingine akiwa na wenzake na moja iliyoorodheshwa kama "labda ilianguka".

Ilipofika mwezi wa Juni 1943, kikosi cha ndege cha VF-10 kikarudi Marekani. Walipokuwa huko, kikosi hicho kikaongezewa silaha za vita na ndege ya aina ya F6F Hellcat. Hellcat ilikuwa ndege bora zaidi ya kivita: kubwa, kasi sana na yenye nguvu nyingi. Vilevile,ilikuwa na risasi na bomu nyingi: risasi 1600 za aina ya 0.5 in(12.7 mm) badala ya zile 1300 za ndege ya Wildcat.

Katika mwezi wa Januari 1944, akiwa Luteni wa daraja la chini, Gordon alirudi vita tena akiwa kwenye meli ya Enterprise. Aliipiga risasi ndege ya aina ya A6M Zero na kuiangusha karibu na Taroa mnamo 29 Januari na 16 Februari akawa mashuhuri kivita alipopiga risasi na kuangusha Zero ingine.

Mnamo 1 Aprili 1944, Gordon alipandishwa cheo akawa Luteni kamili. Katika vita iliyojulikana kama "Marinas Turkey Shoot", Luteni Gordon alipiga risasi ndege ya aina ya Yokosuka D4Y "Judy" iliyokuwa ikijaribu kushambulia ndege za Marekani. Siku iliyofuata , alihusika katika mpango wa kukabiliana na mashambulizi ya ndege za Kijapani. Alipokuwa akisindikiza ndege ya kikosi cha wanamaji, alipiga risasi Zero ingine katika harakati za ulinzi.

Baada ya vita, Gordon aliendelea kufanya kazi na kikosi cha Wanamaji huko Marekani na akawa mmoja katika kikosi cha kwanza kutumia ndege mpya za kivita. Gordon aliendelea kimasomo na akafuzu kutoka Chuo cha Jackson, Hawaii. Alipandishwa cheo kuwa Kapteni mnamo 1 Februari 1962 na akastaafu kutoka kikosi chake katika mwezi wa Julai 1967.

Katika kazi yake, alipewa sifa kwa kuangusha ndege saba za adui zilizothibitishwa, mbili akiwa na wenzake na moja ikaorodheshwa katika orodha ya "labda ilianguka". Alipokea tuzo ya Distinguished Flying Cross yenye nyota mbili za dhahabu, Air Medal yenye nyota tatu za dhahabu, Commendation yenye Combat “V” kwa ndege mbili alizoangusha na wenzake, Navy Unit Citation na tuzo mbili ya Presidential Unit (moja ya kazi yake kwenye Guadalcanal na moja kwa kazi yake kwenye meli ya Enterprise).

Maneno yake[hariri | hariri chanzo]

"Sikuwahi pigana kama mbwa. Kawaida nilikabiliana na ndege kutoka nyuma ama mbele. Hawakutuona tukija kamwe. Hiyo ndiyo njia ya kupigana vita".

Marejeo[hariri | hariri chanzo]