Nenda kwa yaliyomo

Didara, Bisoe na Nor

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Didara, Bisoe na Nor (walifariki Aleksandria mwanzoni mwa karne ya 4) ni kati ya Wakristo wa Misri waliouawa kwa ajili ya imani yao katika dhuluma ya kaisari Diokletian. Ni mama na watoto wake.

Nor au Hor alikuwa askari. Aliteswa sana kabla hajachomwa kwa mkuki.

Bisoe au Besoy au Psoi au Absahi alikatwa kichwa.

Mama yao Didara au Daydara au Didra alikufa wakati wa kuteswa.

Tangu kale wanaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 23 Juni.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.