Nenda kwa yaliyomo

Destiny Etiko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Destiny Etiko
Amezaliwa 12 Agosti 1989 (1989-08-12) (umri 35) jimbo la Enugu, Nigeria
Kazi yake Muigizaji
Miaka ya kazi 2013 – hadi sasa

Destiny Etiko (alizaliwa 12 Agosti 1989) ni mwigizaji wa kike wa Nigeria aliyeshinda tuzo ya mwigizaji chipukizi wa kike mwaka 2016.[1]

Maisha na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Etiko alizaliwa katika kijiji cha Udi, kilichopo jimbo la Enugu, kusini mashariki mwa nchi ya Nigeria.

Etiko alipata elimu ya msingi na sekondari katika jimbo la Enugu. Alipata shahada ya kwanza ya Sanaa ya maonyesho katika chuo kikuu cha Nnamdi Azikiwe. [2]

Etiko alijishughulisha na kazi ya uigizaji filamu kuanzia mnamo mwaka 2011. Alianza kupata umaarufu na kutambulika baada ya kushirikishwa katika filamu iliyojulikana kama Idemili iliyoundwa mwaka 2012 na Ernest Obi na kuachiliwa mwaka 2014. Uhusika wake katika filamu hiyo ilimpelekea kupata tuzo ya mwigizaji chipukizi wa kike mwaka 2016. [2]

Tuzo na Teuzi

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Tuzo Kitengo Matokeo Marejeo
2016 City People Entertainment Awards Muigizaji bora wa kike wa maka alishinda [3]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Tofauti na kile ambacho kimekuwa kawaida katika tasnia ya filamu za Nigeria, ili kufanikiwa katika sanaa ilimlazimu kuhamia jiji la Lagos [4][2] na amekuwa akiishi huko wakati wote wa kazi yake ya uigizaji. Etiko katika mahojiano alithibitisha kwamba alikuwa muathirika wa unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake uliofanyika na watayarishaji wa sinema za kiume ambao ndio wengi zaidi katika uzalishaji wa sinema nchini Nigeria.[5]

Etiko mnamo 2019 alimzawadia mama yake nyumba na kumsifu kwa kuunga mkono uamuzi wake wa kuwa mwigizaji. Baba yake kwa upande mwingine alikuwa amepinga vikali uamuzi wake wa kuwa mwigizaji wakati wa kwanza. Mnamo Mei 2020, alimpoteza baba yake.

Filamu zake

[hariri | hariri chanzo]
  • The prince & I (2019)
  • Heart of Love (2019)
  • My sisters love (2019)
  • Poor Billionaire (2019)
  • Virgin goddess (2019)
  • Queen of love (2019)
  • The Sacred Cowry (2019)
  • The Return of Ezendiala (2019)
  • Barren Kingdom (2019)
  • Pains of the Orphan (2019)
  • Clap of Royalty (2019)
  • The Hidden Sin (2019)
  • Family Yoke (2019)
  • King’s Word (2019)
  • Sound of Evil (2019)
  • My Private Part (2019) as Stella
  • Power of Royalty (2019)
  • Sunset of Love (2019)
  • London Prince (2019)
  • Woman of Power (2019)
  • Tears of Regret (2018)
  • Evil Seekers (2017)
  • Fear of a Woman (2016)
  • 3 Days to Wed (2016)
  • The Storm (2016)
  1. "Nigerian actress, Destiny Etiko: Career, Personal Life, Childhood And Early Life". Within Nigeria (kwa American English). 2019-08-12. Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  2. 2.0 2.1 2.2 "Actress Etiko Destiny stuns in bikinis to mark birthday". Vanguard News (kwa American English). 2015-08-12. Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  3. Showemimo, Adedayo (26 Julai 2016). "Full List Of Winners at 2016 City People Entertainment Awards". Nigerian Entertainment Today. Iliwekwa mnamo 16 Mei 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Etiko Destiny touted with best figure in Nollywood". Vanguard News (kwa American English). 2017-10-29. Iliwekwa mnamo 2019-12-26.
  5. "'Sleeping around is not a guarantee to getting movie roles'". Vanguard News (kwa American English). 2015-04-04. Iliwekwa mnamo 2019-12-26.