Deon Stewardson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Deon Stewardson
Amezaliwa 11 Octoba 1951
Afrika ya Kusini
Amekufa 27 Octoba 2017
Nchi Afrika ya Kusini
Kazi yake Mwigizaji


Deon Stewardson (11 Oktoba 1951 - 27 Oktoba 2017) alikuwa mwigizaji huko Ufalme wa Muungano na Afrika ya Kusini na anajulikana kwa uhusika wake kama Anders Du Plessis katika mfululizo wa tamthilia ya Wild at Heart. Katika tamthiliya zake alizoigiza, saba zilikuwa maarufu huko Ufalme wa Muungano na idadi ya watazamaji walikuwa takribani milioni 7.5 mpaka milioni 10. Tamthiliya yake ya mwisho ilirekodiwa mwaka 2011 na alifanya kazi pamoja na waigizaji kama Hayley Mills. Stewardson pamoja na mkewe Marianne na wakaishi katika eneo la Hartbeespoort Dam Afrika ya Kusini kwa kipindi cha miezi 6 wakitengeneza filamu. Deon Stewardson pia ameonyesha uhusika wake katika filamu ya The Foster Gang na Lethal Woman.[1]

Deon alikuwa mtoto wa mwigizaji Joe Stewardson wa Afrika ya Kusini na kaka wa Matthew Stewardson ambaye alionekana kwenye maonyesho ya Idols South Africa (season 1).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Deon Stewardson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.