Kipanya-miti
Kipanya-miti | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kipanya-miti kahawiachekundu (Dendromus mystacalis)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Vipanya-miti ni wanyama wadogo wa nusufamilia Dendromurinae katika familia Nesomyidae ambao wanafanana na vipanya, lakini vipanya ni wanafamilia wa Muridae. Spishi zote zinatokea Afrika kusini kwa Sahara. Jenasi Dendromus na Steatomys zina usambazaji mkubwa katika Afrika, lakini jenasi nyingine ni dogo na zina sambazaji zilizozuiliwa. Nasaba za jenasi za vipanya-miti bado haina hakika. K.m. Dendromus na Steatomys zina mnasaba mbali kiasi. Leimacomys imepewa juzi nusufamilia yake Leimacomyinae.
Kama jina lao linaashiria vipanya-miti wanaweza kupanda miti sana na spishi nyingi huishi mitini takriban saa zote, isipokuwa spishi za Steatomys (vipanya wanono) ambazo huishi ardhini hasa. Wanyama hawa ni wadogo sana, isipokuwa Kipanya-miti Mkubwa. Rangi yao ni kijivu hadi kahawia na nyeupe chini. Wana mkia mrefu, lakini mkia wa vipanya wanono si sana.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Dendromus insignis, Kipanya-miti milima (Remarkable Climbing Mouse)
- Dendromus kahuziensis, Kipanya-miti wa Mlima Kahuzi (Mount Kahuzi Climbing Mouse)
- Dendromus leucostomus, Kipanya-miti wa Monard (Monard's African Climbing Mouse)
- Dendromus lovati, Kipanya-miti wa Lovat (Lovat's Climbing Mouse)
- Dendromus melanotis, Kipanya-miti masikio-meusi (Grey Climbing Mouse)
- Dendromus mesomelas, Kipanya-miti wa Brant (Brant's Climbing Mouse)
- Dendromus messorius, Kipanya-miti migomba (Banana Climbing Mouse)
- Dendromus mystacalis, Kipanya-miti kahawiachekundu (Chestnut Climbing Mouse)
- Dendromus nyasae, Kipanya-miti wa Kivu Kivu Climbing Mouse)
- Dendromus nyikae, Kipanya-miti misitu (Nyika Climbing Mouse)
- Dendromus oreas, Kipanya-miti wa Kameruni (Cameroon Climbing Mouse)
- Dendromus ruppi, Kipanya-miti wa Rupp (Rupp's climbing mouse)
- Dendromus vernayi, Kipanya-miti wa Vernay (Vernay's Climbing Mouse)
- Megadendromus nikolausi, Kipanya-miti Mkubwa (Nikolaus's mouse)
- Dendroprionomys rousseloti, Kipanya-miti Mahameli (Velvet climbing mouse)
- Leimacomys buettneri, Kipanya-miti wa Togo (Togo mouse)
- Prionomys batesi, Kipanya-miti wa Dollman (Dollman's climbing mouse)
- Malacothrix typica, Kipanya-jangwa masikio-marefu Gerbil Mouse au Long-eared mouse)
- Steatomys bocagei, Kipanya Mnono wa Bocage (Bocage's African Fat Mouse)
- Steatomys caurinus, Kipanya Mnono Magharibi (Northwestern Fat Mouse)
- Steatomys cuppedius, Kipanya Mnono Mdogo (Dainty Fat Mouse)
- Steatomys jacksoni, Kipanya Mnono wa Jackson (Jackson's Fat Mouse)
- Steatomys krebsii, Kipanya Mnono wa Krebs (Krebs's Fat Mouse)
- Steatomys opimus, Kipanya Mnono wa Pousargues (Pousargues's African Fat Mouse)
- Steatomys parvus, Kipanya Mnono Kibete (Tiny Fat Mouse)
- Steatomys pratensis, Kipanya Mnono Nyika (Fat Mouse)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Kingdon, J. 1997. The Kingdon Field Guide to African Mammals. Academic Press Limited, London.
- Musser, G. G. and M. D. Carleton. 2005. Superfamily Muroidea. Pp. 894-1531 in Mammal Species of the World a Taxonomic and Geographic Reference. D. E. Wilson and D. M. Reeder eds. Johns Hopkins University Press, Baltimore.
- Steppan, S. J., R. A. Adkins, and J. Anderson. 2004. Phylogeny and divergence date estimates of rapid radiations in muroid rodents based on multiple nuclear genes. Systematic Biology, 53:533-553.