Kipanya-miti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Malacothrix)
Kipanya-miti
Kipanya-miti kahawiachekundu (Dendromus mystacalis)
Kipanya-miti kahawiachekundu (Dendromus mystacalis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wagugunaji)
Nusuoda: Myomorpha (Wanyama kama panya)
Familia: Nesomyidae (Wanyama walio na mnasaba na buku)
Forsyth Major, 1897
Nusufamilia: Dendromurinae (Wanyama wanaofanana na vipanya-miti)
Alston, 1876
Jenasi: Dendromus A. Smith, 1829

Dendroprionomys Petter, 1966
Leimacomys Matschie, 1893
Malacothrix Wagner, 1843
Megadendromus Dieterlen & Rupp, 1978
Prionomys Dollman, 1910
Steatomys Peters, 1846

Vipanya-miti ni wanyama wadogo wa nusufamilia Dendromurinae katika familia Nesomyidae ambao wanafanana na vipanya, lakini vipanya ni wanafamilia wa Muridae. Spishi zote zinatokea Afrika kusini kwa Sahara. Jenasi Dendromus na Steatomys zina usambazaji mkubwa katika Afrika, lakini jenasi nyingine ni dogo na zina sambazaji zilizozuiliwa. Nasaba za jenasi za vipanya-miti bado haina hakika. K.m. Dendromus na Steatomys zina mnasaba mbali kiasi. Leimacomys imepewa juzi nusufamilia yake Leimacomyinae.

Kama jina lao linaashiria vipanya-miti wanaweza kupanda miti sana na spishi nyingi huishi mitini takriban saa zote, isipokuwa spishi za Steatomys (vipanya wanono) ambazo huishi ardhini hasa. Wanyama hawa ni wadogo sana, isipokuwa Kipanya-miti Mkubwa. Rangi yao ni kijivu hadi kahawia na nyeupe chini. Wana mkia mrefu, lakini mkia wa vipanya wanono si sana.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Kingdon, J. 1997. The Kingdon Field Guide to African Mammals. Academic Press Limited, London.
  • Musser, G. G. and M. D. Carleton. 2005. Superfamily Muroidea. Pp. 894-1531 in Mammal Species of the World a Taxonomic and Geographic Reference. D. E. Wilson and D. M. Reeder eds. Johns Hopkins University Press, Baltimore.
  • Steppan, S. J., R. A. Adkins, and J. Anderson. 2004. Phylogeny and divergence date estimates of rapid radiations in muroid rodents based on multiple nuclear genes. Systematic Biology, 53:533-553.