Nenda kwa yaliyomo

Demba Diawara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Demba Diawara (alizaliwa mnamo mwaka 1931) ni imamu wa msikiti na kiongozi wa kijiji cha Keur Simbara nchini Senegal. Anajulikana kwa uongozi wake katika kuhamasisha jamii za Wabambara kuacha mila za ukeketaji wa wanawake.[1]

Maagizo ya kwanza kutoa katika kijiji cha Senegalse cha Malicounda Bambara kuachana mila za ukeketaji mnamo mwaka 1997.

Diawara alizaliwa mnamo mwaka wa 1931. Yeye ni imamu lakini sasa anajulikana kama kiongozi mkuu wa kijiji cha Keidi Simbara magharibi mwa Senegal.[2]

Kampeni ya Diawara

[hariri | hariri chanzo]

Diawara alikuwa na wasiwasi aliposikia mnamo 1997 kwamba kijiji cha Malicounda Bambara iliwahi kufanya azimio la kusimamisha desturi ya kuteketeza wanawake iliyokuwa sehemu ya utamduni wa Wabambara. Kijiji cha pili Nguerigne Bambara kilifuata mwaka uleule.[3] Diawara alisafiri hadi Malicounda Bambara kueleza wasiwasi zake lakini aliambiwa arudi nyumbani kwanza ajadili na wanawake wa kijiji chake kwanza.[4] Akifuata maagizo hayo, Diawara alijifunza mengi akaona faida ya kubadilisha utamaduni. [5] Wanawake walimwambia mambo ambayo hakuwahi kusikia. Alijua kwamba shemeji yake alishindwa kuzaa akielewa sasa sababu yake ni kuteketezwa. Hakuwahi kuambiwa kwamba kunaleta maumivu makali hakuwahi.[6]

Diawara alitaka kijiji chake kufuata mfano wa majirani lakini aliona tatizo. Watu wa vijiji vingine wangeona mabinti kuwa najisi kama hawakukatwa hadi wasingeolewa.[5] Aliona kwamba angehitaji kushawishi pia vijiji vingine vya kabila lake na kutumia mawasiliani katika ujoo.[7] Alina pia haja ya kusambaza ujumbe huo kwa upole bila kushtaki utamatuni na wafuasi wake.

Diawara pamoja na mpwa wake na mwanamke aliyewahi kuteketeza mabinti katika kijiji chake walianza kuzunguka katika vijiji vingine vya Wabambara na kusambaza ujumbe[8] wakianza kutembelea ndugu za koo za babake na mamake.[9]

Tarehe 14 Februari 1998 wawakilishi 60 kutoka vijiji 13 walikutana huko Diabougou karibu na mpaka wa Mali wakapatana kumaliza desturi ya kuteketeza wanawake (FGC). Waliwakilisha wakazi 8,000.

Juhudi za Diawara ziliendelea na mwaka 1999 vijiji 105 vyenye watu 80,000 viliamua kuachana na desturi ya kuteketeza.

Serikali ya Senegal ilipiga desturi hiyo marufuku lakini mtindo wa Diawara unanekana kuleta matokeo mazuri kuliko kanuni za kisheria pekee.

  1. name=tostan
  2. Demba and the village of Keur Simbara, Rina Jimenez-David, 4 December 2011, Philippine Daily Inquirer, Retrieved 23 December 2015
  3. Bettina Shell-Duncan; Ylva Hernlund (1 Januari 2000). Female "circumcision" in Africa: Culture, Controversy, and Change. Lynne Rienner Publishers. ku. 257–259. ISBN 978-1-55587-995-2.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Geraldine Terry; Joanna Hoare (2007). Gender-based Violence. Oxfam. ku. 74–75. ISBN 978-0-85598-602-5.
  5. 5.0 5.1 Maria Armoudian (23 Agosti 2011). Kill the Messenger: The Media's Role in the Fate of the World. Prometheus Books. ku. 224–225. ISBN 978-1-61614-388-6.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Luc Sindjoun (2010). The Coming African Hour: Dialectics of Opportunities and Constraints. African Books Collective. ku. 160–161. ISBN 978-0-7983-0230-2.
  7. Demba and the village of Keur Simbara, Rina Jimenez-David, 4 December 2011, Philippine Daily Inquirer, Retrieved 23 December 2015
  8. Geraldine Terry; Joanna Hoare (2007). Gender-based Violence. Oxfam. ku. 74–75. ISBN 978-0-85598-602-5.
  9. Ending female genital mutilation, one household at a time, Gannon Gillespie,22 August 2013, The Guardian, Retrieved 21 August 2015
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Demba Diawara kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.