Nenda kwa yaliyomo

Defao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Defao
Jina la kuzaliwa Matumona Defao Lulendo
Amezaliwa (1958-12-31)Desemba 31, 1958
Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Aina ya muziki Soukous, muziki wa dansi
Kazi yake mwimbaji/mtunzi wa nyimbo, mwanamuziki
Ala Sauti, gitaa
Miaka ya kazi 1976 - 2021
Ame/Wameshirikiana na Orchestre Suka Movema, Fogo Stars, Bozi Boziana, Grand Zaiko Wawa, Pepe Felix Manuaku

Francoise Lulendo Matumona (anajulikana kama General Defao; 31 Desemba 1958 - 27 Desemba 2021) alikuwa mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ni miongoni mwa waimbaji wa Kikongo wenye majina makubwa.

Kazi zake za muziki hasa alizifanyia hukohuko kwao Kongo. Alianza kuimba mwaka 1976 kwenye makundi madogomadogo, huko mjini Kinshasa. Waliomvutia kuingia katika muziki kwa kipindi hicho ni Papa Wemba, Nyoka Longo, Gina Efonge Evoloko na waimbaji wanne wa kundi la Zaiko la miaka ya sabiini. Lakini yule hasa aliyemvutia akiimba ni Tabu Ley Rochereau. Tangu mwaka 1991, amenzisha bendi yake mwenyewe, The Big Stars, kwa lengo la kuwa nyota wa Afrika. Alifanya hili kwa kuwa nchini mwao ukishindwa kutimiza jambo fulani watu wanakucheka na huona wivu wengine wakifanikiwa - ndiyo-maana anafanya juhudi kubwa ili tu apate mafanikio.

Hayo yametokea kwa sababu asilimia kubwa wanamuziki wa Kongo hawana subira. Wanataka kila kitu harakaharaka. Sasa hivi katika umri wake miaka hamsini, Defao anachukulia mambo kadiri yanavyokuja na si kwa pupa tena. Anajua ya kwamba, kwake, kibao kitamgeukia. Defao alikufa mnamo Desemba 27, 2021 katika hospitali ya Laquintinie huko Douala, akiwa na umri wa miaka 62, kutokana na Covid-19.

Maisha na muziki

[hariri | hariri chanzo]

Amezaliwa huko mjini Kinshasa mnamo tarehe 31 Desemba 1958 na jina la Matumona Defao Lulendo. Alianza kazi ya muziki mnamo mwaka wa 1976, awali akiwa na Orchestre Suka Movema, halafu baadaye Fogo Stars ikafuatiwa na Korotoro na mwaka wa 1978 Somo West. Mwaka wa 1981 alijiandikisha na kundi jipya kabisa la wakati huo Grand Zaiko Wawa na mpigaji gitaa mashuhuri Pepe Felix Manuaku kabla ya kuungana na Ben Nyamabo katika uanzishaji wa kundi zima la Choc Stars. Defao alifariki mnamo Desemba 27, 2021 katika hospitali ya Laquintinie huko Douala, akiwa na umri wa miaka 62, kutokana na Covid-19.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]

1985

  • Defao of Choc Stars in Paris
  • Defao in Santa feat. Koffi Olomide

1986

  • Defao, Carlyto & Debaba of Choc Stars in Kopalangana *Te - He Wakatsa

1988

  • Defao, Carlyto & Sedjo Ibrahim Ka in Bula
  • Defao of Choc Stars in Niki and Jose
  • Shock Defao Stars in Chagrin Dimone

1989

  • The quiet strength in Defao feat. Koffi Olomide, Pepe Kalle, Luciana Demingongo & Cartlyto
  • Defao in Aime Congolese feat. Papa Wemba Kuru Yaka

1990

  • Defao of Choc Stars in Hitachi

1992

  • Defao & Big Stars in Enguduka
  • Defao & Big Stars in Love School
  • Defao & Big Stars in Jem's

1993

  • Defao & Big Stars in System D

1994

  • Defao & Big Stars in Africa Wealth

Donat

  • Apo & Didi Kikuta

1995

  • Defao & Big Stars in Alvaro
  • Defao & Big Stars in General
  • Defao & Big Stars in Mercy my love
  • Defao & Big Stars in Benson
  • Defao & Big Stars in the Latest Album 95

1996

  • Defao Stars & Big Family Kikuta in 2nd round
  • Defao & Big Stars in Forbidden Love
  • Defao & Big Stars in Phily Mbala akiwa na Dindo Yogo, Reddy Amisi, Luciana Demingongo, Djuna Djanana

'1997

  • Defao & Big Stars in Sala Noki
  • Defao & Big Stars in General

1998

  • Defao & Big Stars in Copinnage feat. Mbilia Bel
  • Defao & Big Stars in Earthquake

1999

  • Defao & Big Stars within 2 Charlots
  • Defao & Big Stars in the War of 100 years

2000

  • Defao in Bana Congo feat. Werrason, Marie Paul, Mbilia Bel
  • Atmosphere in Defao More feat. Manda Chante, Likinga Redo, Alibaba Koffi
  • Nessy Defao in London

2006

  • Defao Nzombo in the Evening

2010

  • Even in Pure Defao

2012

  • Defao in Undertaker

2014

  • Defao in Time is Money akiwa na Gode ​​Lofombo, Celeo Scram, Rogatien Ibambi "Roga Roga-Missile" Sam Tshintu "Che Mint" Manda Chante & Nkumu

2021

  • Byga Nsumbo

DVD na VHS

[hariri | hariri chanzo]

1995

  • Defao & Big Stars dans Alvaro
  • Defao & Big Stars dans le Général
  • Defao & Big Stars dans Pitié mon amour
  • Defao & Big Stars dans Benson
  • Defao & Big Stars dans le Dernier Album 95

1996

  • Defao & Big Stars dans Defao Production Famille Kikuta
  • Defao & Big Stars dans Amour Interdit
  • Defao & Big Stars dans Phily Mbala

1997

  • Defao & Big Stars dans Sala Noki
  • Defao & Big Stars dans le Général

1998

  • Defao & Big Stars dans Copinnage feat. Mbilia Bel
  • Defao & Big Stars dans Tremblement de Terre Clips Inédits

1999

  • Defao & Big Stars dans les 2 Charlots
  • Defao & Big Stars dans la Guerre de 100 ans

2000

  • Defao dans Bana Congo feat. Werrason, Marie Paul, Mbilia Bel
  • Defao dans Ambiance Plus feat. Manda Chante, Likinga Redo, Alibaba Koffi
  • Defao dans Nessy de London

2006

  • Defao dans Nzombo le Soir

2010'

  • Defao dans Pur Encore

2012

  • Defao dans Undertaker

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]