Curtis Frye
Curtis Frye (alizaliwa Vass, Carolina Kaskazini, 20 Oktoba 1951) ni kocha mkuu wa timu ya riadha katika Chuo Kikuu cha South Carolina. Alikua kocha msaidizi kwenye timu ya wanawake ya riadha ya Marekani kwenye michezo ya Olimpiki mnamo mwaka 2004 huko Athens, Ugiriki.
Mbio alizofahamu kabisa ni zile za urukaji viunzi, mbio fupi na zile za kubadilishana. Hizi ndizo pia maeneo ya wajibu wake katika timu ya Olimpiki ya wanawake ya Marekani.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Kabla ya kuhamia Carolina Kusini, Frye alikuwa kocha msaidizi katika Chuo Kikuu cha East Carolina, Chuo Kikuu cha Florida, Chuo Kikuu cha Jimbo la North Carolina na Chuo Kikuu cha North Carolina katika eneo la Chapel Hill.
Akiwa Florida, alikuwa kocha wa Dennis Mitchell, aliyeshinda medali ya shaba katika mbio ya Olimpiki ya 1992 jijini Barcelona.
Akiwa Carolina Kaskazini, alikuwa kocha kwa Marion Jones na Allen Johnson. Johnson bado hutreni na Frye huko Columbia,Carolina Kusini na ni kocha msaidizi wa kujitolea wa Gamecocks.
Akiwa Carolina Kusini, wanariadha wake maarufu ni kama Terrence Trammell,, Demetria Washington, Miki na Lisa Barber, Otis Harris, Aleen Bailey, Lashinda Demus, Natasha Hastings na Tiffany Ross-Williams.
Timu zake zimeshinda katika nafasi za mbele mfululizo katika mashindano ya NCAA na timu ya wanawake ilishinda taji la kitaifa katika Mashindano ya Mabingwa ya Wanawake ya NCAA ya 2002.Hili ndilo taji la kwanza la NCAA katika chuo hicho. Mwaka huo alipewa tuzo ya kocha bora wa kitaifa wa mwaka.
Frye alianzisha kikundi cha Speed Elite kilichokuwa cha wanariadha kama Johnson na Monique Hennaga,kilikuwa na lengo la kushindana katika mashindano ya kitaifa na ya kimataifa na kuyashinda.
Curtis Frye huweka thamani sana katika elimu na huhakikisha kwamba wanafunzi wake wote wanariadha huhitimu kutoka chuo. Kati ya wanariadha karibu 200 aliyekuwa kocha wao katika Chuo Kikuu cha Carolina Kusini,mmoja tu ndiye hakumaliza masomo yake ya shahada ya kwanza na kuhitimu digrii kutoka shule.
Mafanikio
[hariri | hariri chanzo]- 2008 Tuzo ya Amri ya Ikkos
- 2002 Washindi katika Mashindano ya Wanawake ya NCAA
- 1999 & 2002 Mashindano ya Wanawake ya Nje ya SEC
- 1999 & 2002 Kocha wa Wanawake wa Kitaifa wa Mwaka wa USTCA
- 1999 Kocha wa Wanaume wa Kitaifa wa Mwaka USTCA
- 1999 & 2002 Kocha wa Wanawake wa Mwaka SEC
- Katika mwaka wa 2002,alikuwa kocha wa wanariadha walishinda mataji saba ya NCAA na medali nne za dhahabu na moja ya fedha katika Mashindano ya Ubingwa ya Dunia. Aidha,wawili walipewa mataji ya Wanariadha Bora wa Mwaka na mmoja akatuzwa kuwa Mwanariadha-msomi wa Kitaifa wa Wanaume wa Mwaka.
- 2001 Nike Kocha wa Mwaka
- Kocha mkuu wa Wanaume katika Michezo ya Goodwill 2001.
- 1999 Kocha Msaidizi wa Marekani katika Mashindano ya Dunia ya Mabingwa ya Riadha.
- 1997 USOC Field Kocha wa Mwaka
- Kocha msaidizi wa Timu 18 katika Mashindano ya ACC
- Alikuwa kocha wa wanariadha 6 wa Olimpiki walioshinda medali
- Alikuwa kocha wa wanariadha 25 wa Olimpiki 25 (ambao walishinda medali 11)
- Alikuwa kocha wa mabingwa 60 wa NCAA
- Alikuwa kocha wa mabingwa 415 wa Amerika wa NCAA.
- Alikuwa kocha wa Mabingwa 100 wa SEC.
- Alikuwa kocha wa Mabingwa 75 wa ACC.
Baadhi ya wanariadha waliofanikiwa chini ya kocha Curtis Frye
[hariri | hariri chanzo]-
Natasha Hastings
-
Aleen Bailey
-
Terrence Trammell
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Fry's Bio at GamecocksOnline.com Archived 21 Juni 2009 at the Wayback Machine.
- Fry's Bio at USA Track & Field Archived 30 Septemba 2010 at the Wayback Machine.