Kirukanjia wa Afrika
Mandhari
(Elekezwa kutoka Congosorex)
Kirukanjia wa Afrika | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kirukanjia-kipanya misitu (Myosorex varius)
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 3:
|
Virukanjia wa Afrika ni wanyama wadogo wa nusufamilia Myosoricinae katika familia Soricidae wanaofanana na vipanya, lakini virukanjia si wagugunaji (oda Rodentia). Spishi hizi zinatokea Afrika kusini kwa Sahara tu lakini hawa si spishi pekee za Afrika. Kuna spishi nyingi nyingine za virukanjia katika Afrika walio wanafamilia wa nusufamilia Crocidurinae (virukanjia meno-meupe). Hula wadudu na nyungunyungu hasa lakini mbegu na makokwa pia. Meno yao yamechongoka yenye ncha kali. Rangi yao ni nyeusi, kijivu au kahawia.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Congosorex phillipsorum, Kirukanjia-Kongo wa Phillips (Phillips's Shrew)
- Congosorex polli, Kirukanjia-Kongo Mkubwa (Greater Congo Shrew)
- Congosorex verheyeni, Kirukanjia-Kongo Mdogo (Lesser Congo Shrew)
- Myosorex babaulti, Kirukanjia-kipanya wa Babault (Babault's Mouse Shrew)
- Myosorex blarina, Kirukanjia-kipanya Milima (Montane Mouse Shrew)
- Myosorex bururiensis, Kirukanjia-kipanya wa Bururi (Bururi forest shrew)
- Myosorex cafer, Kirukanjia-kipanya Miguu-myeusi (Dark-footed Mouse Shrew)
- Myosorex eisentrauti, Kirukanjia-kipanya wa Eisentraut (Eisentraut's Mouse Shrew)
- Myosorex geata, Kirujanjia-kipanya wa Geata (Geata Mouse Shrew)
- Myosorex gnoskei, Kirukanjia-kipanya Nyika (Nyika Mouse Shrew)
- Myosorex jejei, Kirukanjia-kipanya wa Kahuzi (Kahuzi swamp shrew)
- Myosorex kabogoensis, Kirukanjia-kipanya wa Kabogo (Kabogo mouse shrew)
- Myosorex kihaulei, Kirukanjia-kipanya wa Kihaule (Kihaule's Mouse Shrew)
- Myosorex longicaudatus, Kirukanjia-kipanya Mkia-mrefu (Long-tailed Forest Shrew)
- Myosorex meesteri, Kirukanjia-kipanya wa Meester (Meester's forest shrew)
- Myosorex okuensis, Kirukanjia-kipanya wa Oku (Oku Mouse Shrew)
- Myosorex rumpii, Kirukanjia-kipanya wa Rumpi (Rumpi Mouse Shrew)
- Myosorex schalleri, Kirukanjia-kipanya wa Schaller (Schaller's Mouse Shrew)
- Myosorex sclateri, Kirukanjia-kipanya wa Sclater (Sclater's Mouse Shrew)
- Myosorex tenuis, Kirukanjia-kipanya Mwembamba (Thin Mouse Shrew)
- Myosorex varius, Kirukanjia-kipanya Misitu (Forest Shrew)
- Myosorex zinki, Kirukanjia-kipanya wa Kilima Njaro (Kilimanjaro Mouse Shrew)
- Surdisorex norae, Kirukanjia-fuko wa Aberdare (Aberdare mole shrew)
- Surdisorex polulus, Kirukanjia-fuko wa Mlima Kenya (Mt. Kenya mole shrew)
- Surdisorex schlitteri, Kirukanjia-fuko wa Mlima Elgon (Mt. Elgon mole shrew)