Chuo Kikuu cha Zanzibar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo ya Chuo kikuu cha Zanzibar

Chuo Kikuu cha Zanzibar ni chuo kikuu kilichofunguliwa mwaka 2002 kama chuo kikuu cha kwanza Zanzibar[1] [2], kikiwa kama taasisi binafsi inayodhaminiwa na asasi isiyo ya kiserikali ya Darul Iman Charitable Association.

Kipo eneo la Tunguu katika Wilaya ya kati, kilometa 12 kuanzia Mji wa Zanzibar. Kampasi ya chuo kikuu, ikiwa na jumla ya eneo la kilomita 2 kwa ardhi, ipo miongoni mwa vijiji vitulivu vinavyotazamana na Bahari ya Hindi. Usafiri wa umma (mabasi namba 8, 9, na 10) kutoka Mji wa Zanzibar yatakuleta katika mazingira ya Chuo Kikuu. Chuo kikuu chenyewe kipo nusu maili kutoka barabara kuu.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1994, Al-Haj Aboud Jumbe Mwinyi, Rais wa zamani wa Zanzibar, aliweza kuwashawishi wawakilishi wa taasisi ya Darul Iman Charitable Association (TIK), ambao walikuwa wameweka makazi Dar es Salaam, kujenga chuo cha Ufundi Zanzibar. Ombi lilikubaliwa na ujenzi wa chuo ulianza mwaka 1994 na kukamilika mwaka 1997.

Lengo la kuanzisha chuo cha Ufundi baadaye lilibadilishwa na kuwa la kuanzisha Chuo Kikuu, ikiwa ni ombi la aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Dk Salmin Amour Juma, wakati mchakato wa ujenzi kazi chuo ulipokamilika mwaka 1997. Taasisi ya Darul Iman ilikubali ombi la Serikali ya Zanzibar. Hivyo, Chuo kikuu cha Zanzibar kilifunguliwa rasmi mwezi Aprili 1998. Hii ni taasisi ya kwanza ya elimu ya juu katika Zanzibar.

Malengo ya chuo kikuu cha Zanzibar[hariri | hariri chanzo]

Malengo ya Chuo Kikuu cha Zanzibar kimsingi ni ugunduzi na kuendeleza matumizi ya maarifa, kupata ujuzi, na maendeleo ya akili katika kanda ya Afrika Mashariki kwa lengo la kuandaa wanafunzi kuchangia kikamilifu na kimaadili kama raia wema wa dunia inayobadilika haraka na kuongozwa na teknolojia. Malengo haya sasa hufikiwa kupitia programu ya shahada ya kwanza ya kielimu ambayo ni iliyoundwa kufanya wanafunzi waliohitimu kuwa na uwezo wa kuajiri wenyewe na kuajiri wengine vilevile.

Mipango ya baadaye[hariri | hariri chanzo]

Chuo Kikuu cha Zanzibar kilipangwa kuanza na kitivo cha utawala wa biashara. Kwa kweli, kuenea kwa makampuni ya biashara na hoteli, na upanuzi wa sekta ya utalii nchini kuwa umewashawishi wadhamini wa Darul Iman kuanza Chuo Kikuu cha Zanzibar na kitivo cha Utawala wa Kibiashara kwa lengo kukidhi mahitaji ya haraka ya biashara jamii. Mwaka 1999, Kitivo cha Sheria na Shariah na kilianzishwa mwaka 2002 ya Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii pia kilianzishwa. Katika miaka saba ijayo au hivyo,miundo ya kisasa kabisa itajengwa kwa ajili ya vitivo vingine, yaani - Kitivo cha Sayansi, na Kitivo cha Uhandisi. Vitivo vyote baadae vitaanza kutoa shahada ya kwanza, shahada ya uzamili na Udaktari.

Usajili[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kupata barua ya mpito ya Usajili wa mwaka 1998, Chuo Kikuu cha Zanzibar kimejaribu kwa uwezo wake kutekeleza hatua ya pili na ya tatu, mapendekezo yote yakiletwa na Kamati ya uthamini wa kiufundi ya tume ya usajili wa Elimu ya juu Tanzania. Matokeo yake, Chuo kilipokea cheti cha mpito cha Usajili mwaka 1999, na cheti cha Kamili Usajili tarehe 4 Mei 2000.

Kwa kushirikiana pamoja na Kituo cha Utafiti wa Usimamizi cha Afrika na ulaya (E-AMARC) mjini Maastricht, Uholanzi, Chuo kikuu cha Zanzibar kimeanzisha kituo cha kukuza biashara ndogondogo.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "First university in Zanzibar opens its doors ." New York Amsterdam News (5 Desemba 2002) Vol. 93 Toleo la 49, ukurasa 2.
  2. "Zanzibar." Times Higher Education Supplement (25 Aprili 2003) Toleo 1586, ukurasa10.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Zanzibar kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.