Nenda kwa yaliyomo

Kisiwa cha Chumbe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Chumbe)
Kisiwa cha Chumbe.
Kisiwa cha Chumbe.
Mnara wa taa wa Chumbe.

Kisiwa cha Chumbe ni kati ya visiwa vya mkoa wa Unguja Mjini Magharibi, Zanzibar, nchini Tanzania, ambacho kinapatikana katika Bahari ya Hindi, kilichopo km 13 kusini mwa mji wa Zanzibar kikitazama Fumba Town.

Kisiwa hicho ni kati ya sehemu za kitalii zilizojumuishwa katika maeneo yanayohifadhiwa na kulindwa na Umoja wa Mataifa. Eneo hili lina zaidi ya asilimia 90 ya spishi za Coral katika Afrika ya Mashariki.

Ni makazi ya zaidi ya aina 368 za samaki, kaa wa kwenye minazi, mwewe na pomboo pia wanapatikana katika eneo hili. Pamoja na hayo kuna aina 60 za ndege ambao wanapatikana hapo.

Kisiwa kinatawaliwa na kampuni ya binafsi inayoendesha utalii wa kiekolojia.

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje