Nenda kwa yaliyomo

Chris Dodd

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chris Dodd

Christopher John Dodd (alizaliwa 27 Mei, 1944) ni mwanasheria wa Marekani na mwanasiasa wa chama cha kidemokrasia ambaye aliweza kutumikia kama  seneta kutokea Connecticut kuanzia mwaka 1981 mpaka mwaka 2011. Dodd ni seneta aliyetumikia kwa muda mrefu katika historia ya jimbo la Connecticut. Kabla ya kuwa seneta, alitumikia katika bunge la Wawakilishi wa Marekani kuanzia mwaka 1975 mpaka mwaka 1981.

Dodd ni mwenyeji wa Connecticut na muhitimu katika shule ya Georgetown kule Bethesda, Maryland na katika chuo cha Providence. Baba yake Thomas J. Dodd alikuwa pia ni seneta wa marekani kuanzia mwaka 1959 mpaka mwaka 1971. Chris Dodd alitumikia katika Peace Corps kwa miaka miwili kabla ya kujiunga na chuo kikuu cha sharia cha Louisville na katika kipindi cha masomo ya sheria alitumikia katika jeshi la hifadhi la kimarekani.

Dodd alirudi Connecticut ambapo alishinda uchaguzi wa mwaka 1974 kwa bunge la Wawakilishi wa Marekani kutoka katika jimbo la pili la Connecticut alirudishwa tena mnamo mwaka 1976 na mwaka 1978. Alifaulu kuchaguliwa katika senati ya Marekani mnamo mwaka 1997. Dodd alitumikia kama mwenyekiti wa kamati kuu ya Chama cha Kidemokrasia kuanzia mwaka 1995 mpaka mnamo mwaka 1997. Alitumikia kama mwenyekiti wa kamati ya benki ya seneti kuanzia mwaka 2007 mpaka kufikia kustaafu kwake katika siasa.[1]   mwaka 2006 Dodd alifanya uamuzi  wa kugombea uteuzi wa kidemokrasia wakuwa mgombea uraisi Marekani katika chama cha kidemokrasia, lakini aliweza kujiengua baada ya kuonekana kuzidiwa na baadhi ya washindani.

Januari 2010, Dodd alitangaza kuwa hatagombea tena.[2]  Nafasi ya Dodd iliweza kurithiwa na mwanademokrasia Richard Blumenthal. Badae Dodd aliweza kutumikia kama mwenyekiti na mshawishi wabunge mkuu wa kampuni ya Motion Pictures Association of America (MPAA) kuanzia mwaka 2011 mpaka kufikia mwaka 2017.[3] [4]

Kwenye mwaka 2018, Dodd alirudi katika kazi ya uanasheria na kujiunga na kampuni ya Arnold na Porter. Zaidi ya kuwa mwanachama wa ReFormers Caucus ya "IssueOne", Dodd alikuwa mshauri wa karibu wa raisi Joe Biden na akatumikia katika kamati ya kumteua mgombea kwa nafasi ya makamu wa raisi wa Marekani.[5][6]

  1. "Financial Markets Highlights November 2007". Financial Market Trends. 2007 (2): 11–25. 2007-11-22. doi:10.1787/fmt-v2007-art12-en. ISSN 0378-651X.
  2. "Washington Post Monthly Poll, March 2010". ICPSR Data Holdings. 2011-05-05. Iliwekwa mnamo 2022-08-08.
  3. "Washington Post Monthly Poll, March 2010". ICPSR Data Holdings. 2011-05-05. Iliwekwa mnamo 2022-08-08.
  4. "Los Angeles Times Festival of Books Royce Hall, UCLA", I Told You So, OR Books, ku. 13–26, iliwekwa mnamo 2022-08-08
  5. George Peel, Hon. (2017-10-10), "The Caucus Takes Charge", The Tariff Reformers, Routledge, ku. 151–164, ISBN 978-1-315-09889-0, iliwekwa mnamo 2022-08-08
  6. "CROWN-PRINCE RETRIEVED: LIFE AT CUSTRIN NOVEMBER 1730-FEBRUARY 1732", The Works of Thomas Carlyle, Cambridge University Press, ku. 342–406, 2010-11-11, iliwekwa mnamo 2022-08-08
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chris Dodd kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.