Choman Hardi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Choman Hardi, 2023.

Choman Hardi (alizaliwa 1974) ni mshairi, mkalimani na mchoraji wa lugha ya Kikurdi.

Maisha ya nyuma[hariri | hariri chanzo]

Amechapisha Diwani tatu za mashairi katika lugha Kikurdi, pia amechapisha diwani mbili za mashairi ya Kiingereza, ambayo ni Life for Us (Bloodaxe Books, 2004) na Considering the Women (Bloodaxe Books, 2015), ambapo yaliorodheshwa katika tuzo mnamo mwaka 2016. Nakala zake zimeonekana katika ushairi wa kisasa katika tafsiri [1]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Choman alikuwa mwenyekiti wa Exiled Writers Ink na aliandaa warsha za uandishi wa ubunifu kwa ajili ya baraza la Uingereza nchini Uingereza, Ubelgiji, Jamhuri ya Czech na India . Alikuwa mshairi katika makazi ya kituo cha waandishi cha Moniack Mhor (Scotland), Villa Hellebosch (Ubelgiji), Hedgebrook Women Writers' Retreat (Marekani) na The Booth (Shetland). Kama mtafiti wa kitaaluma amekuwa msomi anayetembelea katika kituo cha utafiti wa Multiethnic (Chuo Kikuu cha Uppsala), Zentrum Moderner Orient (Berlin) na Department of Humanities (Chuo Kikuu cha Amsterdam). Kati ya mwaka 2009 na 2011 alikuwa mwanachama mshiriki mwandamizi wa Chuo cha St Anthony's, Oxford. Mnamo mwaka 2014 alirudi katika jiji la nyumbani la Sulaimani kuchukua wadhifa katika Chuo Kikuu cha Amerika cha Iraqi (AUIS), na kuwa mwenyekiti wa idara ya Kiingereza mnamo 2015.

Vitabu[hariri | hariri chanzo]

  • — (1996), Return with no memory (in Kurdish), Denmark, ISBN 87-984331-6-4 
  • — (1998), Rûnakîy sêberekan : şîʻir (Light of the Shadows), Kitêbî Rabûn, 14. (in Kurdish), Rabûn, ISBN 9789197335447 
  • — (2000), Light Mirrors and Shadows: Poems, OCLC 427634821 
  • — (2004), Life for Us, Bloodaxe Books, ISBN 9781852246440 
  • — (2011), Gendered Experiences of Genocide: Anfal Survivors in Kurdistan-Iraq, Voices in development management., Farnham, Surrey, ISBN 978-0754694335 
  • — (2015), Considering the Women, Bloodaxe Books, ISBN 9781780372785 

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Kurdish Women Refugees: Obstacles and opportunities", in Forced Migration and Mental Health, pp149–168, 2005.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Choman Hardi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.