Chokowe ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia ya Scolopacidae. Nje ya majiri ya kuzaa huonekana hasa karibu na maji (bahari, maziwa, mito) lakini spishi chache huonekana mbali na maji (k.m. Tryngites subruficollis). Takriban spishi zote hutaga mayai chini tundrani kwa kanda za akitiki za Ulaya, Asia na Amerika. Hula wadudu, gegereka na nyungunyungu.