Cheryl Foster

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Cheryl Foster mnamo 2018

Cheryl Fozzy Foster (alizaliwa 4 Oktoba 1980) alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu na kwa sasa ni mwamuzi wa nchini Welisi.[1] Alishikilia rekodi ya mchezaji bora katika timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Welisi mwaka 2009, alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa mwaka 1997. [2]

Katika ngazi ya klabu Foster alichezea kwa muda wa miaka tisa katika klabu ya wanawake ya Liverpool, alicheza katika misimu miwili ya kwanza ya ligi ya FA WSL mwaka 2011 na 2012 . Baadae alisajiliwa na klabu ya Doncaster Rovers Belles mnamo Januari 2013, kabla ya kustaafu kwake.

Kazi ya uamuzi[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kuamua kutoongeza muda wake wa kucheza kama mchezaji mnamo 2013, Foster badala yake alianza mazoezi kama mwamuzi . [3] Alikuwa mwamuzi msaidizi katika fainali ya Kombe la Wanawake la Welisi katika msimu wa 2013-14 . [4] Mnamo Desemba 2015, katika msimu wake wa tatu kama mwamuzi, Foster alitajwa kwenye orodha ya kimataifa ya FIFA . [5]

Mnamo 18 Agosti 2018, alikua mwamuzi wa kwanza mwanamke kucchezesha katika mechi za Ligi Kuu ya Welisi . [6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Players". Liverpool Ladies FC. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 March 2010. Iliwekwa mnamo 4 May 2010.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  2. "Ladies football: Chester schoolteacher Cheryl Foster become most capped player in Welsh women's football history". The Chester Chronicle. Iliwekwa mnamo 4 May 2010.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "Golden girl Foster will train as ref and coach", North Wales Daily Post, 14 May 2014. 
  4. "Brown fires Cardiff Met to Women's Cup Glory", 13 April 2014. 
  5. "Welsh referees make FIFA international list", 3 December 2015. 
  6. "WELSH PREMIER". 19 August 2018. Iliwekwa mnamo 19 August 2018.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Cheryl Foster kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.