Chama cha Skauti Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Skauti wakisafisha gari.

Chama cha Skauti Tanzania (Kiingereza Tanzania Scouts Association, kwa kifupi: TSA) ni shirika la skauti nchini Tanzania; lilianzishwa mwaka 1917 na kusajiliwa mwaka 1963 na kuwa mwanachama wa Shirika la Harakati za Skauti Duniani, hadi mwaka 2010 shirika hili lilikuwa na wanachama 538,933.[1]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Skauti ilianza kujilikana Zanzibar mwaka 1912 na baadae kuingia Tanganyika mwaka 1917 na kuwa mwanachama wa Shirika la Harakati za Skauti Duniani mnamo mwaka 1912. Mnamo mwaka 1984 Tanzania iliandaa mkutano wa kimataifa wa sita wa Skauti barani Afrika.

Serikali ya Sweden imekuwa ikifadhili chama hicho kwa miaka kadhaa sasa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Some statistics". World Organization of the Scout Movement. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 April 2010. Iliwekwa mnamo 30 March 2010.  Unknown parameter |df= ignored (help); Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)