Skauti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Viongozi wakipokea mtoto katika chama cha skauti huko Mexico City, Mexico.
Scouting for boys 1 1908.jpg

Skauti (kutoka neno la Kiingereza "scout") ni mtoto, kijana au msichana anayewajibika katika chama cha kimataifa, akivaa sare kama ya askari mdogo na kukaa katika safu.

Pia ni chama kisicho cha kiserikali kinachomjenga kijana katika maadili mema na ya kujituma na kusaidia watu katika maisha yao.

Chama hicho hakibagui vijana kwa msingi wa jinsia, umri, dini, rangi wala kabila.

Skauti huhitajika kuwepo kwa kila shule za sekondari duniani.

Mwanzilishi wa chama cha skauti duniani (1907) aliitwa Robert Baden-Powell (18571941) kutoka Uingereza. Lengo lake lilikuwa kusaidia vijana kukua vizuri pande zote (mwili, nafsi na roho) ili hatimaye wawe raia wema katika jamii.

Kanuni za skauti[hariri | hariri chanzo]

 • 1. Heshima ya skauti ni kuaminika.
 • 2. Skauti ni mzalendo kamili.
 • 3. Skauti ni mtu wa kufaa na kusaidia wengine.
 • 4. Skauti ni rafiki kwa wote na ndugu kwa kila mtu aliye skauti na asiye skauti.
 • 5. Skauti ni mwenye adabu kamili.
 • 6. Skauti ni mwenye huruma kwa viumbe.
 • 7. Skauti ni mtiifu kamili.
 • 8. Skauti ni mchangamfu daima.
 • 9. Skauti ni safi katika mawazo, maneno na matendo yake.
 • 10. Skauti ni mwangalifu wa mali zake na za wengine pia.
 • 101/2. Skauti si mjinga na mjinga si skauti (Kanuni hii imetolewa na mwalimu Julius K. Nyerere)
Mwanzilishi wa chama cha skauti