Nenda kwa yaliyomo

Carlo Agostini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Carlo Agostini (22 Aprili 1888 – 28 Desemba 1952) alikuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki la Italia. Alihudumu kama Patriarki wa Venezia kuanzia 1949 hadi kifo chake, na alifariki muda mfupi baada ya kutangazwa kwa uteuzi wake kuwa kardinali mwaka 1952.

Alizaliwa katika mji wa San Martino di Lupari, Carlo Agostini alisoma katika seminari ya Treviso, na alipewa daraja ya upadri na Askofu Andrea Longhin mnamo 24 Septemba 1910. Baada ya hapo, aliendelea na masomo yake Roma, na kupata udaktari wa katika falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thomas Aquinas (Angelicum) na shahada ya udaktari teolojia kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriani mwaka 1913. [1]

  1. Milestones. Time. January 5, 1953.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.