Nenda kwa yaliyomo

Mpapai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Carica papaya)
Mpapai
(Carica papaya)
Mpapai
Mpapai
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Brassicales (Mimea kama kabichi)
Familia: Caricaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mpapai)
Jenasi: Carica
L.
Spishi: C. papaya
L.

Mpapai ni mti wa familia Caricaceae ambao unazaa mapapai.

Mti huo unatoka Meksiko lakini siku hizi hukuzwa kila mahali katika ukanda wa tropiki kwa sababu matunda yake hupendwa sana.

Ni mti mrefu wenye shina la urefu wa mita 5 mpaka 10, wenye majani yaliyojipanga yaliyojizungusha na kujishikiza juu kwenye shina la mti, shina kwa upande wa chini huwa na makovu mengi kuonesha sehemu ambayo majani yalikuwa. Majani ya mpapai ni makubwa sm 50 – 70 kwa upana, maua yake ni madogo na hutokea sehemu yalipochomoza majani, hutengeneza tunda papai lenye urefu wa sm 15- 45, na upana wa sm 10 – 30.

Picha

Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mpapai kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.