Buba Baldeh
Buba Baldeh | |
Amezaliwa | Buba Sidiki Michael Baldeh 11 Novemba 1953 Basse Mansajang, Upper River Division, Gambia |
---|---|
Amekufa | 9 Julai 2014 Dakar, Senegal |
Chama cha kisiasa | APRC |
Ndoa | Alioa wake 2 |
Watoto | 8 |
Buba Sidiki Michael Baldeh (Novemba 11, 1953 - Julai 9, 2014)[1] alikuwa mwanasiasa na mwandishi wa habari wa Gambia. Alikuwa mhariri mkuu wa zamani wa The Daily Observer, gazeti la kila siku la Gambia, tangu mwaka 2000 hadi 2002.[2] Baldeh pia alikuwa mwanachama wa zamani wa Bunge la Kitaifa la Gambia kutoka mwaka 1982 hadi 1985 na 1987-1994 wakati wa jamhuri ya kwanza ya Gambia.Buba baadaye aliendelea kutumikia nyadhifa kadhaa baada ya mapinduzi ya 1994 hadi alipogombana na Rais wa Jamhuri ya Gambia Yahya Jammeh.
Maisha ya mapema
[hariri | hariri chanzo]Baldeh alizaliwa Basse Mansajang, Upper River Division, Gambia.[2] Baba yake, Michael Baldeh, alikuwa mwanachama wa Baraza la Wawakilishi la Gambia, (sasa inaitwa National Assembly of the Gambia) wakati wa Gambia Colony na Protectorate | Kipindi cha ukoloni wa Briteni.[2]
Kazi ya mapema
[hariri | hariri chanzo]Baldeh alianza kazi yake akifanya kazi kama mkuu wa wilaya ya Gambia kutoka mwaka 1972 hadi 1977. Baadaye aliteuliwa jukumu la mkurugenzi wa mradi wa Kampeni ya Uhuru kujikomboa kwa Njaa mnamo mwaka 1977.[1]
Kazi ya kisiasa
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 1982, Baldeh alichaguliwa kwenye Baraza la Wawakilishi la Gambia lakini alifukuzwa nje mnamo mwaka 1985. Alichaguliwa tena kwenye Baraza la Wawakilishi mnamo mwaka [1987]] na kuwa katibu wa Wizara ya Afya mnamo 1990. [1] Baldeh pia alishikilia nafasi ya Waziri wa Vijana na Michezo kutoka mwaka 1992 hadi 1994. Utawala wake kama mbunge ulimalizika na 1994 Gambia coup d'état.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 Perfect, David (27 Mei 2016). Historical Dictionary of The Gambia (tol. la 5th). ku. 49–50. ISBN 9781442265226. Iliwekwa mnamo 23 Oktoba 2016.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 "Gambia: Buba Baldeh Dies in Senegal", The Point (the Gambia), AllAfrica.com, July 10, 2014. Retrieved on July 31, 2014.
- ↑ Touray, Suntou. "Gambian Exiled Politician Buba Baldeh Has Fallen", Radio Kairo, July 9, 2014. Retrieved on July 31, 2014. Archived from the original on 2015-11-21.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Buba Baldeh kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |